Breaking

Post Top Ad

https://refpasrasw.world/L?tag=d_1066073m_7669c_&site=1066073&ad=7669

Friday, July 23, 2021

Makamu Wa Rais Kuanza Ziara Ya Kikazi Mtwara


 Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango, leo Julai 23, 2021 anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tano mkoani Mtwara.

Makamu wa Rais akiwa mkoani Mtwara anatarajiwa kushiriki misa ya kumbukizi ya mwaka mmoja wa kifo cha hayati Rais wa awamu ya tatu Benjamin William Mkapa katika Kijiji cha Lupaso Wilaya ya Masasi.

Aidha Makamu wa Rais anatarajiwa kuzindua  stendi ya mabasi Wilaya ya Nanyumbu, soko la kisasa la matunda na mbogamboga la Jidah wilayani Masasi, kuzindua kiwanda cha kubangua korosho Wilaya ya Newala pamoja na kuzungumza na wananchi katika maeneo mbalimbali atakayotembelea.

Katika hatua nyingine Makamu wa Rais anatarajiwa kuweka jiwe la msingi Hospitali ya Kanda ya kusini iliopo Wilaya ya Mtwara na baadaye kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara utakaofanyika katika viwanja vya sabasaba Mtwara mjini.


Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages