Picha : CHAMA CHA WAFANYAKAZI WA SERIKALI ZA MITAA 'TALGWU' SHINYANGA CHAPATA VIONGOZI WAPYA…WAMPONGEZA RAIS SAMIA

Msimamizi wa Uchaguzi wa viongozi wa TALGWU mkoa wa Shinyanga Bi. Shani Kibwasari ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma TALGWU makao Makuu TALGWU 
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) mkoa wa Shinyanga, Dkt. Martine Dotto Mazigwa 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) Mkoa wa Shinyanga wamefanya uchaguzi wa viongozi mbalimbali ambapo wamemchagua Dkt. Martine Dotto Mazigwa kuwa Mwenyekiti wa TALGWU Mkoa wa Shinyanga kutumikia nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano.

Uchaguzi huo umefanyika leo Jumamosi Julai 24,2021 wakati Mkutano Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) Mkoa wa Shinyanga uliofanyika katika ukumbi wa Shy Park Hotel Mjini Shinyanga.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi, Msimamizi wa Uchaguzi Bi. Shani Kibwasari ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma TALGWU makao Makuu  amesema wagombea nafasi ya Mwenyekiti wa TALGWU mkoa wa Shinyanga walikuwa Dkt. Martine Dotto Mazigwa, Nyalali Thomas Ndaki, Robert Kaunda Sospeter ambapo Dkt. Martine Mazigwa ameibuka mshindi wa kiti hicho. 

Nyalali Ndaki amechaguliwa kuwa Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa, Nunya Chege Mjumbe wa  Kamati ya Utendaji taifa pamoja na viongozi wengine wa nafasi mbalimbali.

Awali akifungua Mkutano Mkuu wa TALGWU Mkoa wa Shinyanga, Mweka Hazina wa TALGWU taifa, Siston Mizengo amewataka wanachama wa TALGWU kuhakikisha wanakiunga mkono chama hicho ili kiweze kuendelea kuwahudumia wanachama wake.

Mizengo amesema hakuna haki bila wajibu hivyo wanachama na watumishi wa TALGWU wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanatimiza wajibu wao ili hata pale wanapodai haki basi hiyo haki iwe inastahili.

Mizengo ametumia fursa hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza kwa vitendo ahadi anazotoa kwa wafanyakazi akibainisha kuwa Rais Samia anatekeleza kile anachosema.

“Tunatumia nafasi hii kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza kwa vitendo ahadi aliyoitoa kwenye Siku ya Mei Mosi mwaka 2021 jijini Mwanza, aliahidi mambo mengi kwa watumishi ikiwemo kuwapandisha madaraja,nyie wafanyakazi ni mashahidi si mmeona?, ee kwa hiyo tuna Rais ambaye anasema halafu anatekeleza”,amesema Mizengo.

“Mimi ninavyojua nchi yetu ni ya wakulima na wafanyakazi, tujitahidi kumuunga mkono Mheshimiwa Rais Samia na tunamuunga mkono  Rais Samia kwa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa,kufanya kazi kwa nidhamu,kufanya kazi kwa kuhakikisha kwamba taifa letu linasonga mbele”,ameongeza Mizengo.

“Kingine alichotufanyia Rais Samia si mnakumbuka wale waliokopa mikopo ya elimu ya juu,ile tozo ya asilimia 6 aliifuta, lakini pia kodi kwenye mishahara yetu Mhe. Rais Samia alipunguza asilimia moja kutoka asilimia 9 hadi 8 ambapo zamani kodi ilikuwa inafikia hadi asilimia 16”,amesema.

Hata hivyo amesema mafanikio yote yaliyopatikana siyo kwamba yamepatikana from No where ni kwa jitihada za viongozi wenu mliowachagua kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali wakiwemo wa TUCTA katika kuisukuma serikali ili kuhakikisha inatekeleza yale iliyoyaahidi kwa wafanyakazi.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI

Mweka Hazina wa TALGWU taifa, Siston Mizengo akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) Mkoa wa Shinyanga uliofanyika leo Jumamosi Julai 24,2021 katika ukumbi wa Shy Park Hotel Mjini Shinyanga. Mkutano huo umekwenda sanjari na uchaguzi wa viongozi wa TALGWU. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mweka Hazina wa TALGWU taifa, Siston Mizengo akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) Mkoa wa Shinyanga uliofanyika leo Jumamosi Julai 24,2021 katika ukumbi wa Shy Park Hotel Mjini Shinyanga. Mkutano huo umekwenda sanjari na uchaguzi wa viongozi wa TALGWU.
Awali Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) Mkoa wa Shinyanga, Maximilian Lugemba akizungumza kwenye Mkutano huo uliofanyika leo Jumamosi Julai 24,2021 katika ukumbi wa Shy Park Hotel Mjini Shinyanga. 
Katibu wa TALGWU Mkoa wa Shinyanga, Ally Ernest akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) Mkoa wa Shinyanga uliofanyika leo Jumamosi Julai 24,2021 katika ukumbi wa Shy Park Hotel Mjini Shinyanga. 
Kidana Milando akisoma taarifa ya Kazi na Fedha kwenye Mkutano Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) Mkoa wa Shinyanga uliofanyika leo Jumamosi Julai 24,2021 katika ukumbi wa Shy Park Hotel Mjini Shinyanga. 
Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) Mkoa wa Shinyanga, Maximilian Lugemba  na waliokuwa viongozi wa TALGWU mkoa wa Shinyanga wakijiuzulu kupisha uchaguzi wa viongozi wapya.
Mweka Hazina wa TALGWU taifa, Siston Mizengo akizungumza wakati wa uchaguzi wa Viongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) Mkoa wa Shinyanga.
Msimamizi wa Uchaguzi wa TALGWU mkoa wa Shinyanga Bi. Shani Kibwasari ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma TALGWU makao Makuu akitangaza utaratibu wa uchaguzi wa viongozi leo wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) Mkoa wa Shinyanga uliofanyika katika ukumbi wa Shy Park Hotel Mjini Shinyanga. 
Afisa Kazi wa TALGWU mkoa wa Mwanza, Bi. Sabina akitoa mwongozo wa uchaguzi wa Viongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) .
Aliyekuwa Mgombea wa Nafasi ya Uenyekiti wa TALGWU mkoa wa Shinyanga , Bi. Regina Shija Maneno akitangaza kujitoa katika kinyang'anyiro hicho.
Wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) mkoa wa Shinyanga wakijiandaa kuomba kura.
Dkt. Martine Dotto Mazigwa akiomba kura kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) mkoa wa Shinyanga.
Nyalali Thomas Ndaki akiomba kura kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) mkoa wa Shinyanga
 Robert Kaunda akiomba kura kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) mkoa wa Shinyanga
Sospeter Nyamuhanga akiomba kura kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) mkoa wa Shinyanga.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) mkoa wa Shinyanga wakipiga kura kuchagua viongozi wao

Zoezi la kuhesabu kura likiendelea
k
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) wakiimba wimbo wa Mshikamano bila kugusana mikono.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) wakiimba wimbo wa Mshikamano bila kugusana mikono.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) wakiwa ukumbini.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments