BENKI YA EQUITY (T) YAZINDUA HUDUMA MPYA ZA KUTUMA FEDHA KIMATAIFA



• Kupitia Huduma za “Equity ni Moja” Wateja Benki ya Equity Tanzania  sasa wanaweza kufanya miamala yao katika matawi yote ya Benki ya Equity Congo DRC, Kenya, Uganda, Rwanda, Sudani ya Kusini kama wapo nyumbani.



• Kupitia huduma mpya ya SADCC- SIRESS wateja wa Benki ya Equity wanaweza  kufanya miamala kwenda na kutoka katika nchi  SADC kwa gharama ya DOLA 10 tu bila kujali kiwango.



Dar es Salaam, Jumanne tarehe 27 Julai 2021. Benki ya Equity Tanzania leo imeingiza sokoni la huduma mbili mpya za utumaji fedha kimataifa  zinazolenga kuingusha Tanzania na nchi nyingine za Afrika. Huduma hizo ni “Equity ni Moja” ” ambayo inawawezesha Wateja Benki ya Equity Tanzania  kufanya miamala yao katika matawi yote ya Benki ya Equity Congo DRC, Kenya, Uganda. Pia Huduma ya SADCC-SIRESS INAYOWAWEZESHA wateja wa Benki ya kufanya miamala kwenda na kutoka katika nchi  SADC kwa gharama ya DOLA 10 tu bila kujali kiwango.


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity (T) Robert Kiboti alisema: "Tunajivunia kuendelea kuwa kiungo cha kuwaunganisha watanzania na mataifa mengine ya Afrika kupitia mfumo wetu mahiri wa utumaji na upokeaji fedha. Huduma zetu za “EQUITY NI MOJA” inafungua milango kwa Wateja wa Benki ya Equity kuweka fedha, kupokea fedha na kufanya malipo katika tawi lolote la Benki ya Equity nchini Kenya, Uganda, Rwanda, Sudan Kusini, na Kongo DRC kama wako nyumbani. Kifupi, kila lilipo tawi la Benki ya Equity, nje na ndani ya Tanzania, mteja wetu atakuwa nyumbani. Wale wanao fanyabiashara nchi za Kenya, DRC, Uganda, Rwanda na Sudan ya Kusini sasa hawahitaji kubeba fedha taslimu. Kusudi la msingi la bidhaa hii ni kutoa suluhisho kwa wateja wa Equity kuzifikia amana zao na kufanya miamala  kwa urahisi popote katika mtandao wetu wa matawi. "alisema Bw. Kiboti.

Kulingana na MD, huduma nyingine ni suluhisho la utumaji  na upokeaji fedha ndani ya eneo la SADC ijulikanayo kama  (SIRESS). "Huu ni mfumo wa kidigitali wa ufanyaji miamala ya kibenki kwa nchi wanachama wa SADC yaani Angola, Botswana, Comoro , Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Eswatini, Lesotho, Madagaska, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Seychelles, Afrika Kusini, Tanzania, Zambia, na Zimbabwe. Kupitia huduma hizi, wateja wa Benki ya Equity wataweza kufanya miamala ya kutuma na kupokea fedha kupitia mtandao wetu kwa uharaka na gharama nafuu ya Dola 10 tu kwa muamala bila kujali kiasi kilichotumwa" anasema MD.

Wafanyakazi wa Equity Bank wakipozi kwa picha 



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments