ZU YAENDELEA KUNG'ARA MAONYESHO YA (TCU)



Chuo kikuu Cha Zanzibar, ZANZIBAR UNIVERISTY (ZU) Cha Tanzania visiwani kimeendelea kung'ara kwenye maonyesho ya kumi na sita (16) yanayoandaliwa na tume ya vyuo vikuu Tanzania.

Dr .Salama Yusuf ambaye ni muadhili Mkuu wa chuo hicho wakati wa mazungumzo yake  leo Julai 28,2021  amesema wanawakaribisha wanafunzi mbalimbali na wa jinsia zote kufika chuoni kwao.

Amesema kwenye maonyesho hayo wanafanya udahili na inakuwa rahisi kwa mzazi au mwanafunzi kufanyiwa udahili kwenye banda lao..

Aidha Dr. Salama aliwashauri waandaaji wa Maonyesho hayo kuyaboresha zaidi kwa sababu ni msaada mkubwa kwa wazazi ama wanafunzi,

Alisema pia (ZU)ni chuo kizuri chenye walimu wazuri na mwanafunzi akimaliza chuoni hapo anakuwa mbobezi wa suala ambalo alilisomea.

Aidha Alisema kutokana na wimbi la tatu (3)la Uviko-19 Zanzibar University inakabiliana sana kwani kuna sehemu maalumu yenye maji tiririka na sabuni

Alisema wanapokuwa sarasani wanawaweka anafunzi kwa umbali kidogo na hata mwalimu anahakikisha wanafunzi wote wamevaa barakoa

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments