MWILI WA MAREHEMU ANNA MGHWIRA KUZIKWA JUMATATU ARUSHA - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Saturday, July 24, 2021

MWILI WA MAREHEMU ANNA MGHWIRA KUZIKWA JUMATATU ARUSHA


Mwili wa aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, na mgombea Urais nchini Tanzania kupitia Chama cha ACT-Wazalendo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, Anna Elisha Mghwira unatarajiwa kuzikwa nyumbani kwake jijini Arusha Jumatatu Julai 26 ,2021.

Mghwira alifariki dunia Julai 22,2021 katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru jijini Arusha alikokuwa akipatiwa matibabu.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai amesema mkoa huo umebeba jukumu la kuandaa mazishi ya Mghwira.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages