RC MAKALLA AAGIZA MABASI YOTE KUSHUSHA ABIRIA STENDI YA MBEZI | MALUNDE 1 BLOG

Friday, July 9, 2021

RC MAKALLA AAGIZA MABASI YOTE KUSHUSHA ABIRIA STENDI YA MBEZI

  Malunde       Friday, July 9, 2021

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amelielekeza Jeshi la Polisi kuhakikisha kuanzia Sasa Mabasi yote yanashusha na kupakia abiria kwenye kituo kikuu cha Mabasi cha Mbezi Louis.

RC Makalla amesema hayo wakati alipotembelea kituo hicho na kusikiliza kero na changamoto mbalimbali za Wafanyabiashara kituoni hapo.

Amesema Serikali inatambua kituo kimoja pekee Cha Mabasi ambacho ni Mbezi na uwekezaji uliofanyika ni mkubwa hivyo hakuna maana kama kila mmiliki wa mabasi atakuwa na kituo chake kupakia na kushusha abiria.

Aidha RC Makalla ameelekeza uongozi wa Stendi hiyo kuweka utaratibu wa baadhi ya Mabasi kushusha abiria kwenye eneo la kulaza magari ambapo kuna Banda la Mamalishe ili kuchochea biashara.

Kuhusu changamoto ndogondogo zilizojitokeza kituoni hapo, RC Makalla ameelekeza Viongozi wa Halmashauri ya Ubungo na kituo kuzipatia ufumbuzi wa haraka.

Mhe.Makalla pia ameelekeza Wafanyabiashara kituoni hapo wapangwe Katika utaratibu mzuri na bora kuendana na hadhi ya kituo. 

Wakati huohuo RC Makalla ametembelea Soko la Machinga lililopo pembezoni mwa Stendi hiyo na kutaka Wafanyabiashara wote wahamishiwe sokoni hapo na uchunguzi ufanyike kwa wale waliopatiwa vibanda kwa upendeleo na kujuana ambapo Wafanyabiashara hao wamesema wapo tayari kuhamia sokoni apo na wamechoka kufanya biashara barabarani.

Amemuelekeza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kuweka utaratibu wa Daladala kushusha abiria sokoni apo ili kuchagiza biashara.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post