RAIS SAMIA AMTEUA MSANII NIKK WA PILI KUWA DC KISARAWE, JOKATE APELEKWA TEMEKE, MWIGIZAJI CHOPA MCHOPANGA ALAMBA RORYA | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, June 20, 2021

RAIS SAMIA AMTEUA MSANII NIKK WA PILI KUWA DC KISARAWE, JOKATE APELEKWA TEMEKE, MWIGIZAJI CHOPA MCHOPANGA ALAMBA RORYA

  Malunde       Sunday, June 20, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Msanii Nickson Simon John maarufu Nikk wa Pili kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani.

DC mteule Nikk wa Pili anachukua nafasi ya Jokate Mwegelo ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke.

Vilevile, Rais Samia amewateua baadhi ya waliokuwa wabunge lakini kwa sababu mbalimbali wakashindwa kurejea bungeni. Wateule hao ni Joshua Nassari (Bunda), Halima Bulembo (Muheza) na Peter Lijualikali (Nkasi).


Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Mwigizaji Juma Chikoka maarufu Chopa Mchopanga kuwa Mkuu wa Wilaya ya Rorya Mkoa wa Mara.

Pia Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Basilla Mwanukuzi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga, Basilla aliwahi kuwa Miss Tanzania 1998.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post