DC MBONEKO AIBUKIA MNADANI NA SOKO LA MACHINGA , ATAKA WAFANYABIASHARA KUCHUKUA TAHADHARI YA CORONA | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, June 22, 2021

DC MBONEKO AIBUKIA MNADANI NA SOKO LA MACHINGA , ATAKA WAFANYABIASHARA KUCHUKUA TAHADHARI YA CORONA

  Malunde       Tuesday, June 22, 2021

 

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiwasili kwenye Mnada wa Tinde wilayani Shinyanga, kuhamasisha usafi wa mazingira, pamoja na wafanyabiashara kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.

Na Marco Maduhu, Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, amefanya ziara kwenye mnada wa Tinde wilayani Shinyanga, pamoja na Soko la Machinga lililopo eneo la CCM mjini Shinyanga, na kuwahamasisha wafanyabiashara kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.

Mboneko amefanya ziara hiyo leo Jumanne Juni 22,2021, kuhamasisha usafi wa mazingira pamoja na kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona kwa kuweka vyombo vya kunawia mikono kwa sabuni na maji tiririka, pamoja na kuvaa barakoa.

Akizungumza na wafanyabiashara hao, amesema ni vyema wananchi wakaendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya virusi hivyo, ili wabaki kuwa salama.

“Kuanzia sasa naagiza minada yote wilayani Shinyanga na masoko, ziwekwe ndoo za maji tiririka na sabuni kila eneo, pamoja na kuvaa barakoa, ili kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona," alisema Mboneko.

"Katika kipindi cha virusi vya Corona awamu iliyopita, nchi ilibaki kuwa salama kwa sababu watu walizingatia kunawa mikono mara kwa mara kwa sabuni na maji tiririka, na kuvaa barakoa, hivyo ni vyema tukaendeleza utamaduni huo," aliongeza.

Katika hatua nyingine aliwataka wananchi wote, kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona, kwa kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima, kutoshikana mikono, na kuvaa barakoa ili wawe salama.

Nao baadhi ya wafanyabiashara hao akiwamo Selemani Mwarabu, walisema watazingatia suala hilo la kuchukua tahadhari ya kujinga na virusi hivyo vya Corona kwa kufuata masharti ya wataalam wa afya.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza na wafanyabiashara katika Mnada wa Tinde wilayani Shinyanga na kuwataka wachukue tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona, kwa kuweka vifaa vya kunawa mikono mara kwa mara na kuvaa barakoa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza na wafanyabiashara katika Mnada wa Tinde wilayani Shinyanga na kuwataka wachukue tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona, kwa kuweka vifaa vya kunawa mikono mara kwa mara na kuvaa barakoa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara katika Mnada wa Tinde juu ya kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.
Elimu ya kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona ikiendelea kutolewa.
Elimu ya kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona ikiendelea kutolewa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akikagua kifaa cha kunawa Majitiririka katika Soko la Machinga eneo la CCM na kukuta kifaa hicho hakina maji ndani yake.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akinawa kwa sabuni na Majitiririka katika Soko la Machinga CCM na kuwataka wafanyabiashara wa soko hilo kunawa mikono mara kwa mara, ili kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona, kushoto ni Mwenyekiti wa soko hilo Boniphace Petro.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiwa kwenye Soko la Machinga eneo la CCM Mjini Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiendelea kuhamasisha wafanyabiashara katika Soko la Machinga lililopo eneo la CCM Mjini Shinyanga kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.
Awali Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiwasili katika Mnada wa Tinde wilayani Shinyanga, kuhamasisha masuala ya usafi wa mazingira na uchukuaji wa tahadhari juu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post