Tanzia : MTANGAZAJI MAARUFU FREDWAA AFARIKI DUNIA...POLISI WAELEZA CHANZO | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, June 12, 2021

Tanzia : MTANGAZAJI MAARUFU FREDWAA AFARIKI DUNIA...POLISI WAELEZA CHANZO

  Malunde       Saturday, June 12, 2021

Mtangazaji Fred Fidelis maarufu kama Fredwaa amefariki dunia leo Jumamosi Juni 12, 2021 saa 8 mchana  katika ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Kawe Jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni Ramadhani Kingai amesema chanzo cha ajali hiyo ni ulevi na kwamba wanamshikilia dereva wa gari hilo.

“Inaonekana dereva alikuwa amelewa wakati akiendesha gari liliacha njia na kuingia mtaroni eneo la Tanganyika Packers karibu na sehemu ambayo Mchungaji Boniphace Mwamposa huwa anatoa neno, mtangazaji, Fredwaa alifariki ila dereva tunamshikilia” amesema Kingai.

Amesema kwa mujibu wa taarifa hata Fredwaa hakuumia ila inaonekana alipata mshituko kwani dereva hajaumia.

Fredwaa alijizolea umaarufu katika kipindi chake cha asubuhi pale Radio Free Africa jijini Mwanza, ambapo pamoja na mambo mengine alikuwa na segment inaitwa Vodacom Top Five.

Fredwaa baada ya kuhamia Clouds Fm akitokea RFA alikuwa akisikika sana katika kipindi cha asubuhi Power Breakfast, akiungana na Mbwiga, Gerald Hando, Bonge na wengine.

Wakati wa uhai wake, Fredwaa pia amewahi kufanya kazi Times Fm.

R.I.P Fredwaa
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post