Picha : MAFUNZO KWA WAANDISHI WA BLOGS & ONLINE TV YAFUNGWA....WAOMBA SHERIA ZIREKEBISHWE

 Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Deogratius Nsokolo.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mafunzo ya siku tatu kwa Waandishi wa Habari Mtandaoni (Online Media Journalists, Bloggers and Editors) yaliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) kwa lengo la kuwajengea uwezo kuhusu Sheria mbalimbali zinazohusu Tasnia ya Habari ili waweze kuripoti kwa weledi zaidi kuhusu Haki za binadamu yamefungwa huku wakiiomba Serikali kuzifuta sheria zote zinazodaiwa kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari.

Mafunzo hayo yalianza Jumatatu Mei 10,2021 katika ukumbi wa Nashera Hoteli mkoani Morogoro yakikutanisha pamoja waandishi wa habari mtandaoni kutoka Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar.

Waandishi hao wa habari wanaoendesha Blogs na Online Tv wamesema wamekuwa wakishindwa kufanya kazi vizuri kutokana na uwepo wa baadhi ya sheria ambazo siyo rafiki kwa waandishi wa habari kuiomba serikali iondoe/ ibadilishe kandamizi zinazoathiri uhuru wa vyombo vya habari.

Wamezitaja baadhi ya changamoto wanazokutana nazo kuwa ni pamoja na gharama kubwa za kusajili mitandao ya kijamii,kukamatwa na kuharibiwa vifaa vyao,vitisho, faini na adhabu kubwa kwa vyombo vya habari vinavyokiuka sheria na kanuni na kwamba bado gharama Bando (Vifurushi vya Intaneti) hazijashuka hali inayosababisha wakati mwingine washindwe kuingia mtandaoni.

Wamesema wana imani kubwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu hivyo sheria zibadilishwe ili uhuru wa vyombo vya habari uenziwe na viongozi watakaofuata.

Akifunga mafunzo hayo leo Jumatano Mei 12,2021 Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari (UTPC), Deogratius Nsokolo kutokana na uandishi wa habari kubadilika kwa sababu ya watu wengi kutegemea mitandao ya kijamii kupata habari upo umuhimu wa Kuunda Taasisi (Online Association) kwa ajili ya waandishi wa habari mtandaoni ili wajisimamie wenyewe.

Aidha amewataka waandishi wa habari kujiendeleza kielimu na kujisimamia, kufanya utafiti kabla ya kuandika ili waandike habari zenye ubora huku akiwasisitiza kuongeza juhudi za kuandika habari uchunguzi.

"Lakini pia niwasihi mchukue tahadhari mara zote mnapotekeleza majukumu yenu, tusiwe wepesi wa zawadi kwa sababu siyo kila mtu anafurahia anapoandikwa",ameongeza Nsokolo.

Rais huyo wa UTPC pia amewataka waandishi wa habari ambao hawajajiunga na Klabu za Waandishi wa Habari zilizopo kila mkoa wajiunge na amesisitiza kuhusu umuhimu wa waandishi wa habari kuwa na bima za afya akisema kinga ni bora kuliko tiba.

Mratibu wa THDRC, Onesmo Olengurumwa amesema kupitia mafunzo hayo ya siku tatu yamewajengea uwezo waandishi wa habari wa mtandaoni kuhusu masuala mbalimbali ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi zaidi kwa sababu watu wengi wamehamia mtandaoni.

Olengurumwa amewasihi Waandishi wa habari waendelee kuandika kuhusu maboresho ya sheria za habari hali ambayo itasaidia kumfanya Mhe. Rais Samia Suluhu kuona umuhimu wa kubadilisha sheria zinazolalamikiwa ili kuwe na uhuru wa vyombo vya habari.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
 Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Deogratius Nsokolo akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa Waandishi wa Habari Mtandaoni (Online Media Journalists, Bloggers and Editors) yaliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) kwa lengo la kuwajengea uwezo kuhusu Sheria mbalimbali zinazohusu Tasnia ya Habari. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Olengurumwa akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya siku tatu kwa Waandishi wa Habari Mtandaoni (Online Media Journalists, Bloggers and Editors) yaliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) kwa lengo la kuwajengea uwezo kuhusu Sheria mbalimbali zinazohusu Tasnia ya Habari.

Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji TCRA, Dkt. Philip Filikunjombe akizungumza kwenye mafunzo kwa Waandishi wa Habari Mtandaoni (Online Media Journalists, Bloggers and Editors) yaliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) kwa lengo la kuwajengea uwezo kuhusu Sheria mbalimbali zinazohusu Tasnia ya Habari.
Jaji Mstaafu Robert Makaramba akizungumza kwenye mafunzo kwa Waandishi wa Habari Mtandaoni (Online Media Journalists, Bloggers and Editors) yaliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) kwa lengo la kuwajengea uwezo kuhusu Sheria mbalimbali zinazohusu Tasnia ya Habari.
Wakili wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) Leopold Mosha akizungumza kwenye mafunzo kwa Waandishi wa Habari Mtandaoni (Online Media Journalists, Bloggers and Editors) yaliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) kwa lengo la kuwajengea uwezo kuhusu Sheria mbalimbali zinazohusu Tasnia ya Habari.
Afisa Programu wa Idara ya Sheria na Msaada wa Haraka - Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Paul Kisabo akizungumza kwenye mafunzo kwa Waandishi wa Habari Mtandaoni (Online Media Journalists, Bloggers and Editors) yaliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) kwa lengo la kuwajengea uwezo kuhusu Sheria mbalimbali zinazohusu Tasnia ya Habari.
Waandishi wa Habari Mtandaoni (Online Media Journalists, Bloggers and Editors) wakiwa kwenye mafunzo yaliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC)yenye lengo la kuwajengea uwezo kuhusu Sheria mbalimbali zinazohusu Tasnia ya Habari.

Waandishi wa Habari Mtandaoni (Online Media Journalists, Bloggers and Editors) wakiwa kwenye mafunzo yaliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) yenye lengo la kuwajengea uwezo kuhusu Sheria mbalimbali zinazohusu Tasnia ya Habari.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments