BALOZI BATILDA BURIANI ATEULIWA KUWA KATIBU TAWALA MKOA WA SHINYANGA | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, May 30, 2021

BALOZI BATILDA BURIANI ATEULIWA KUWA KATIBU TAWALA MKOA WA SHINYANGA

  Malunde       Sunday, May 30, 2021

 

Balozi Dk. Batilda Buriani

Na Shinyanga Press Club Blog
Leo Mei 29, 2021 Balozi Dk. Batilda Buriani ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga akichukua nafasi ya Albert Msovela ambaye amehamishiwa mkoa wa Mara.

Balozi Dk. Batilda kabla ya uteuzi huo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan mwaka 2015 - 2016 na Kenya mwaka 2012 - 2015.

Pia amekuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia mwaka 2000 hadi 2010 kabla ya kuangushwa kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na Godbless Lema wa Chadema katika jimbo la Arusha Mjini.
 
Katika kipindi chake cha ubunge, aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto ambayo kwa sasa ni Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Vilevile, akawa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) wakati wa serikali ya awamu ya nne.

Balozi Dk. Batilda Buriani
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post