VIGOGO YANGA WATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA TFF BAADA YA KUITWANGA TANZANIA PRISONS 1-0


Vigogo,Yanga SC wamefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Tanzania Prisons Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.

Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji Mburkinabe Yacouba Sogne dakika ya 54 akimalizia pasi ya kiungo Mrundi, Said Ntibanzokiza.

Yanga inaungana na Rhino Rangers ya Tabora, Biashara United ya Mara, Mwadui FC ya Shinyanga na Azam FC ya Dar es Salaam pia kuwa timu zilizotinga Nane Bora hadi sasa.

Michuano hiyo itaendelea kesho kwa mechi kati ya Dodoma Jiji FC na KMC Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na Simba SC na Kagera Sugar Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam wakati keshokutwa JKT Tanzania watamenyana na Namungo FC Uwanja wa Jamhuri, Dodoma kukamilisha Hatua ya 16 Bora.

 Chanzo - Binzubeiry blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments