TMA YASEMA KIMBUNGA JOBO KIMEKUWA HAFIFU | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, April 24, 2021

TMA YASEMA KIMBUNGA JOBO KIMEKUWA HAFIFU

  Malunde       Saturday, April 24, 2021


Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema kimbunga Jobo kimepungua nguvu kwa haraka baada ya kuingia katika mazingira yenye mzunguko wa upepo kinzani.

Taarifa iliyotolewa na TMA leo Jumamosi Aprili 24, 2021  imeeleza kuwa kimbunga hicho kimekuwa hafifu na kinasafiri kwa kasi ya kilometa 18 kwa saa baharini tofauti na spidi ya kilometa 60 kwa saa iliyokuwa imetabiriwa awali.

TMA imesema kimbunga hicho kilichopo Bahari ya Hindi kwa sasa kipo umbali wa kilomita 200 mashariki mwa kisiwa cha Mafia.

“Kimbunga hafifu cha Jobo kinatarajiwa kusababisha vipindi vya mvua kubwa katika maeneo machache hususan ya ukanda wa Pwani kadri kinavyosogea nchi kavu kwa siku ya leo Aprili 24 na kesho Aprili 25, 2021,” inaeleza taarifa hiyo.

Maeneo yanayotarajiwa kupata athari za moja kwa moja ni pamoja na mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani ikiwemo kisiwa cha Mafia, Dar es Salaam pamoja na kisiwa cha Unguja.

Aidha TMA imetahadhalisha kuwa uwepo wa kimbunga hafifu baharini, unatarajiwa kusababisha mawimbi makubwa.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post