SPIKA NDUGAI AWATAKA WABUNGE WAISHAURI SERIKALI KUHUSU UNUNUZI WA NDEGE
Thursday, April 08, 2021
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amewataka wabunge kuchangia Mpango wa Taifa wa Maendeleo kwa kuishauri Serikali kama iendelee na mpango wake wa kununua ndege au isitishe hadi itakapoweka mambo sawa.
Ndugai amesema hayo bungeni mjini Dodoma leo Alhamisi Aprili 8, 2021 kabla kuchangia Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo (2021/22 hadi 2025/26) uliosomwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba.
Amesema Shirika la Ndege (ATCL) limepata hasara ya Sh60 bilioni, hivyo wabunge wanatakiwa kuishauri Serikali wakati wakichangia mpango huo kama iendelee na mpango wa kuongeza ununuzi wa ndege au wasitishe kwanza hadi watakapoweka mambo sawa.
Amewataka wabunge hao kushauri pia katika ununuzi wa mabehewa kwa ajili ya uendeshaji wa reli ya kisasa (SGR) kama ni vyema yakanunuliwa na Serikali au ununuzi ukafanywa na wabia wa sekta binafsi.
Amesema zipo nchi zinafanya uwekezaji wa miundombinu ya reli na suala la mabehewa linafanywa na wawekezaji binafsi.
Amewataka wabunge kutumia nafasi hiyo kuishauri Serikali na wasisubiri kukosoa wakati inapokosea.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com
🚧🚦 Usiendeshe gari lako bila Mafunzo na Leseni halali_ 📲 Wasiliana nasi sasa: wa.me/255740273285 Unahitaji nini? 🚘 Unataka kujifunza udereva wa magari na kupata Cheti? 📄 Una cheti unataka kupata Leseni? 🔄 Unajua kuendesha lakini huna cheti wala leseni na unataka refresh upate cheti? 🛣️ Una nyaraka zote muhimu lakini unahitaji kujifua zaidi barabarani? ✅ Una Leseni bila cheti na unataka renew? 🌍 Tupo mikoa yote Tanzania hadi vijijini! 📞 Tupigie sasa: 0769 763 285
Social Plugin