Serikali kuajiri walimu 6000 ifikapo Juni | MALUNDE 1 BLOG

Friday, April 9, 2021

Serikali kuajiri walimu 6000 ifikapo Juni

  Malunde       Friday, April 9, 2021


 Serikali ya Tanzania imesema itaajiri walimu wapya 6,000 wa Shule za Msingi na Sekondari ifikapo Juni 2021 ili kujaza nafasi zilizoachwa na walimu waliofariki au kustaafu kazi.

Ahadi hiyo imetolewa leo Ijumaa Aprili 9, 2021 na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) David Silinde wakati akijibu swali la msingi la mbunge wa Njombe Mjini (CCM) Deodatus Mwanyika.

Mbunge huyo amehoji Serikali inachukua hatua gani kumaliza tatizo la upungufu wa Walimu nchini hasa Shule zilizopo maeneo ya Vijijini.

Akijibu swali hilo Silinde amesema  Ofisi ya Tamisemi kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia itaajiri walimu wapya 6,000 wa Shule za Msingi na Sekondari ifikapo Juni mwaka huu ili kujaza nafasi zilizoachwa na walimu waliofariki ama kustaafu kazi.

Amesema Tamisemi imekuwa ikifanya uhamisho wa ndani kwa kuwahamisha walimu waliozidi hasa kwenye maeneo ya mijini na kuwapanga kwenye shule zenye uhaba mkubwa wa walimu hasa zilizopo maeneo ya vijijini.

“Serikali itaendelea kuajiri na kuwapanga walimu kwenye shule za msingi na sekondari hasa zenye mahitaji makubwa kwa kadri ya upatikanaji wa fedha,”amesema.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post