SERIKALI YATANGAZA KUSITISHA BEI MPYA ZA BANDO 'VIFURUSHI' VILIVYOZUA GUMZO LEO

Kufuatia malalamiko na mjadala mkubwa mara baada ya kutangazwa kwa bei mpya za vifurushi ambapo matarajio ya wengi ilikuwa ni kushuka kwa gharama hizo leo Aprili 2,2021, Serikali imetangaza kusitisha kutumika kwa gharama hizo hadi hapo itakapotangazwa baadaye.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Semu Mwakyanjala, amesema matumizi ya bei mpya ya vifurushi yamesitishwa kwa muda akieleza kuwa uamuzi huo utahusu vifurushi vya data pekee huku vile vya ujumbe mfupi wa maneno na kupiga zitaendelea kama ilivyotangazwa leo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments