MWANDISHI WA HABARI AVUNJA VUNJA SIMU ILIPOMZINGUA AKIENDELEA NA SEMINA MTANDAONI 'Zoom'

Dunia ina mambo ndivyo unaweza kusema!! Katika hali isiyotarajiwa Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Nipashe Marco Maduhu maarufu 'Tajiri la Kisukuma’ amevunja simu yake ya mkononi 'Smartphone' baada ya simu hiyo kugoma kukamata mtandao na kuzimika mara kwa mara wakati akiendelea na semina mtandaoni kupitia mtandao wa Zoom.

Tukio hilo lililozua gumzo la aina yake katika ofisi ya waandishi wa habari (Shinyanga Press Club) Mjini Shinyanga limetokea leo Jumanne Aprili 13,2021 saa saba na dakika 40 mchana.

Mashuhuda wa tukio hilo wameiambia Malunde 1 blog kuwa wakati Maduhu akiendelea na semina mtandaoni tangu saa tatu asubuhi, simu yake ilikuwa inazima na kukata mtandao mara kwa mara na kumfanya ashindwe kufuatilia kwa ufanisi zaidi mafunzo yaliyokuwa yanaendelea kwenye semina kwa waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kupitia mtandao Zoom yaliyoandaliwa na shirika la Internews.

Wamesema kutokana na hali hiyo,ilipofika saa saba na dakika 40 Maduhu aliibamiza chini simu hiyo na kuipasua pasua kisha kutoka nje na kuitupa huku akisema haiwezekani kuendelea na simu inayoleta usumbufu wakati anafanya mambo ya maana.

Akizungumza na Malunde 1 blog, Marco Maduhu amesema amelazimika kuvunja simu hiyo kwa sababu ilikuwa inamkwamisha kuendelea na semina yake Zoom hivyo haoni sababu ya kuendelea na simu hiyo.

"Simu imeniletea ujinga ni bora kununua simu nyingine tu, haiwezekani nafanya mambo ya msingi halafu simu inaleta ujinga", amesema Maduhu

Muonekano wa simu ya Marco Maduhu baada ya kuvunjwa

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments