MWILI WA FLAVIANA KIFIZI KUWASILI NA KUAGWA KESHO SHINYANGA....WADAU WAFIKA SHUWASA KUSAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, April 21, 2021

MWILI WA FLAVIANA KIFIZI KUWASILI NA KUAGWA KESHO SHINYANGA....WADAU WAFIKA SHUWASA KUSAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO

  Malunde       Wednesday, April 21, 2021


Flaviana Kifizi enzi za uhai wake
****
Mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi aliyefariki dunia Aprili 20,2021 wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam unatarajiwa kuwasili Mkoani Shinyanga na kuagwa nyumbani kwake Lubaga katika Manispaa ya Shinyanga kesho Alhamis Aprili 22,2021.

Kwa mujibu wa Taarifa kutoka Uongozi wa SHUWASA, mwili wa marehemu Flaviana Kifizi utawasili mkoani Shinyanga kesho Alhamisi Aprili 22,2021 majira ya saa tano asubuhi baada ya kupokelewa katika uwanja wa ndege jijini Mwanza ukitokea jijini Dar es salaam.

Mara baada ya mwili wa marehemu Flaviana Kifizi kuwasili nyumbani kwake Lubaga (nyuma ya Shy Park Hotel) Mjini Shinyanga, ratiba ya ibada kumuombea  marehemu itaendelea ikifuatiwa na salamu mbalimbali za rambirambi pamoja na kuaga mwili wa marehemu.

 Baada ya zoezi la kuaga mwili wa marehemu, taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu kwa ajili ya mazishi jijini Mwanza zitaendelea.
Wakazi wa Shinyanga  akiwemo Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko na Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Ntobi wamefika katika ofisi za SHUWASA kwa ajili ya kutoa pole na faraja kwa watumishi wa SHUWASA pamoja na kusaini kitabu cha maombolezo ambacho kimewekwa na uongozi wa SHUWASA kwa ajili ya wananchi na wadau wa SHUWASA kuomboleza kifo cha Bi. Flaviana Kifizi.
Sehemu iliyoandaliwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) na kuweka Kitabu cha Maombolezo ya aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA, Bi Flaviana N. Kifizi katika ofisi za SHUWASA kwa ajili ya wadau mbalimbali kutoa salamu za pole na rambirambi
  
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akisaini Kitabu cha Maombolezo ya aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA, Bi. Flaviana N. Kifizi katika ofisi za SHUWASA leo Aprili 21,2021
Mkurugenzi wa KASHWASA , Mhandisi Joshua Mgeyekwa akisaini Kitabu cha Maombolezo ya aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA, Bi. Flaviana N. Kifizi katika ofisi za SHUWASA leo Aprili 21,2021
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Albert Msovela akisaini Kitabu cha Maombolezo ya aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA, Bi. Flaviana N. Kifizi katika ofisi za SHUWASA leo Aprili 21,2021
Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Shinyanga Mhe. Emmanuel Ntobi akisaini Kitabu cha Maombolezo ya aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA, Bi. Flaviana N. Kifizi katika ofisi za SHUWASA leo Aprili 21,2021
Mjumbe wa bodi ya SHUWASA, Ziporah Pangani akisaini Kitabu cha Maombolezo ya aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA, Bi. Flaviana N. Kifizi katika ofisi za SHUWASA leo Aprili 21,2021
Mkurugenzi wa Malunde 1 blog, Kadama Malunde akisaini Kitabu cha Maombolezo ya aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA, Bi. Flaviana N. Kifizi katika ofisi za SHUWASA leo Aprili 21,2021
Mkurugenzi wa Kampuni ya Gven Wear, Grace Mng'ong'o akisaini Kitabu cha Maombolezo ya aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA, Bi. Flaviana N. Kifizi katika ofisi za SHUWASA leo Aprili 21,2021
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (Patrobas Katambi), Bw. Samwel Jackson akisaini Kitabu cha Maombolezo ya aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA, Bi. Flaviana N. Kifizi katika ofisi za SHUWASA leo Aprili 21,2021

 Soma pia
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post