AUAWA KWA KUPIGWA CHUPA NA MWENYEKITI WA KITONGOJI KAHAMA


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Mwanaume aliyejulikana kwa jina la Daud Lubambula (49) mkazi wa kijiji cha Kidana kata ya Ushetu wilayani Kahama ameuawa kwa kupigwa na chupa kichwani na kwenye mkono wa kulia na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ikindika kata ya Kidana Andrew Adam.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema tukio hilo limetoa Aprili 18,2021 majira ya saa nne usiku  katika kitongoji  cha Ikindika, kijiji cha Kidana, kata ya Ushetu,tarafa ya Dakama, wilaya ya kipolisi Ushetu na mkoa wa Shinyanga.

 “Daud  Lubambula aliuawa kwa kupigwa na chupa kichwani na kwenye mkono wa kulia na mtuhumiwa huyo Andrew Adamu, hali iliyopelekea kuvuja damu nyingi na kupoteza maisha wakati akipatiwa matibabu katika kituo cha afya Ushetu”,amesema Kamanda Magiligimba.

Amesema chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi  uliotokana na ulevi kati ya marehemu na mtuhumiwa  wakiwa kwenye kilabu cha pombe za kienyeji.

Ameeleza kuwa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linatamfuta mtuhumiwa Andrew  Adamu ambaye ni Mwenyekiti wa kitongoji cha Ikindika, mkazi wa kitongoji cha Ikindika kwa kosa la mauaji.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga anatoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo ili kufanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments