ECLA AFRICA CONSULT KUTOA MAFUNZO YA KUANDAA MAHESABU KWA MFUMO WA IPSAS


Meneja Ubia wa ECLA Africa Consult, Lauden Cheyo 
**

Na Mwandishi Wetu.

TAASISI ya ECLA Africa Consult  yenye makao makuu yake Jijini Dar es Salaam, inayojihusisha na masuala ya ukaguzi, ushauri wa kifedha na kodi  inatarajia kuendesha kwa vitendo mafunzo ya siku tano kwa wahasibu na wakaguzi  kutoka NGO's, taasisi za Kidini na  mashirika ya serikali.

Aidha mafunzo  yatahusisha mbinu ya kuandaa taarifa za fedha (financial statements)  kwa kutumia mfumo wa IPSAS (IPSAS framework).

Mafunzo hayo yameandaliwa kufuatia maamuzi ya Bodi ya wahasibu na wakaguzi, ya 22 June 2020 kubadili mfumo wa kuandaa taarifa za kifedha kutoka IFRS (International Financial Reporting Standards) kwenda IPSAS (International Public Sector Accounting standards)  kwa NGOs, Taasisi za dini na Mashirika.

Akizungumza juu ya mafunzo hayo Meneja Ubia  wa ECLA Africa Consult,  Lauden Cheyo, alisema kuwa, mafunzo hayo yanatarajiwa kufanyika  kuanzia 12 Aprili hadi 16 Aprili, mwaka huu katika hoteli ya Regency Park , iliyopo Mikocheni Jijijini Dar es Salaam.

"ECLA Africa Consult, tayari tumefungua milango kuanzia  Aprili Mosi mwaka huu kwa washiriki kujiunga na mafunzo haya kwa vitendo  kwa kulipia kiasi cha Shilingi za kitanzania Milioni moja (Mil.1000000)" ,alisema Cheyo  na kuongeza kuwa

"Nafasi bado zipo kwa mshiriki kuweza kulipia kupitia benki ya CRDB akaunti namba 0150554143800, jina la akaunti Ecla Africa Consult."

Aidha Cheyo  alieleza kuwa, washiriki watapata wasaa wa kupata mafunzo hayo ya kibobezi na mwisho wa mafunzo hayo  washiriki wote  watatunukiwa vyeti maalum.

Aidha, washiriki pia wanaweza kuwasiliana na waandaji hao moja kwa moja kupitia mawasiliano yao +255762148095 ama +255713040994.

Pamoja na mambo mengine  Cheyo alijinasibu kuwa Kampuni ya ECLA Africa Consult inaamini mafunzo hayo yataleta tija kwa washiriki kwa kuwawezesha kuandaa taarifa za fedha zinazokidhi viwango vya mfumo wa IPSAS.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments