ASKOFU AJUTIA KUCHOVYA ASALI YA MKE WA ASKOFU MWENZAKE...AMLAUMU SHETANI



Ntagali alisimamishwa kazi ya kuhudumu kama askofu mwezi Januari mwaka huu baada ya kubainika kwamba alikuwa na uhusiano Judith Tukamuhabwa. Picha: The Observer
***
Askofu Mkuu mstaafu wa kanisa la Kiangilikana nchini Uganda, Stanley Ntagali ameomba msamaha hadharani baada ya kukiri kwamba alichovya asali (alishiriki ngono) na mke wa Askofu mwezake.

Ntagali alisimamishwa kazi ya kuhudumu kama askofu mwezi Januari mwaka huu baada ya kubainika kwamba alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke wa mwenyewe aliyetambulika kwa majina kama Judith Tukamuhabwa.

Ntagali ambaye alitangaza kwamba aliokoka mwaka wa 1974, alikiri kwamba alipotoshwa na shetani kutekeleza kitendo hicho na anaamini Mungu na waumini watamsamehea.

 "Mimi nilimkubali Mungu mwaka wa 1974 siku ya Krismasi, nampenda Mungu na nitazidi kumtumikia, najua Mungu pia ananipenda, Najutia kujiingiza katika uzinzi na kwa sasa naomba msamaha mbele ya Mungu na pia ningependa kanisa linisamehe," Askofu huyo alisema.

 " Askofu wenzangu, kaka, dada zangu katika kristu, naomba mnisamehe, maaskofu wote dunia naomba msamaha na ningependa kuendelea kumtumikia Yesu," Aliongezea Ntagali. 

Kwenye habari zingine, Judith alikuwa amedai kwamba kabla ya kuwa mpenzi wa askofu Ntagali, alikuwa amewasilisha kortini ombi la kutaka kumpa mumewe talaka mwezi Disemba 2020.

 Judith alidai kwamba mumewe alikuwa mkatili, hakuwa anamheshimu na hangestahimili maisha waliokuwa wakiishi.

 Mwanamke huyo na mumewe walioana kwenye harusi ya kifahari katika kanisa la Rugarama Cathedral mjini Kabale Disemba 15, 2018 siku chache baada ya askofu mumewe kufiwa na mkewe.

 CHANZO - TUKO NEWS

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments