WAZIRI MKUU WA ISRAEL BENJAMIN NETANYAHU AJIZUIA KUTUMIA ANGA YA SAUDI ARABIA AKIHOFIA SHAMBULIZI LA MAKOMBORA | MALUNDE 1 BLOG

Monday, March 15, 2021

WAZIRI MKUU WA ISRAEL BENJAMIN NETANYAHU AJIZUIA KUTUMIA ANGA YA SAUDI ARABIA AKIHOFIA SHAMBULIZI LA MAKOMBORA

  Malunde       Monday, March 15, 2021


Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema alizuiwa kusafiri kwenda Umoja wa Falme za Kiarabu kupitia anga ya Saudi Arabia wiki iliyopita kutokana na kitisho cha kushambuliwa kwa kombora na waasi wa Iran walioko Yemen.

 Kauli hiyo imetolewa jana Jumamosi baada ya Netanyahu wiki iliyopita kuahirisha ziara yake kwenye Umoja wa Falme za Kiarabu, kufuatia mzozo na jirani yake Jordan ambayo imefungia kwa muda ndege ya waziri mkuu huyo kutumia anga lake. 

Waziri mkuu huyo pia alishindwa kutumia anga ya Saudi Arabia akisema kulikuwa na changamoto wiki moja iliyopita, akikusudia shambulizi la kombora la hivi karibuni lililofanywa na waasi wa Houthi wa nchini Yemen. 

Hata hivyo Netanyahu hakutoa maelezo ya kina kuhusu matamshi hayo wala kueleza iwapo ndege yake ilikuwa ikilengwa na wanamgambo wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post