RPC DEBORA MAGILIGIMBA ASHINDA TUZO YA MWANAMKE KINARA UONGOZI TAASISI ZA UMMA KANDA YA ZIWA 2021..TAZAMA PICHA


Usiku wa Jumapili Machi 07, 2021 zimetolewa Tuzo za Mwanamke Kinara Kanda ya Ziwa Mwaka 2021 kwenye Kongamano la 'Women Round Table' lililofanyanyika Gold Crest Hotel jijini Mwanza. Tuzo hizo ni sehemu ya kutambua jitihada za wanawake katika kuchochea maendeleo.

Katika Kongamano hilo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba alitangazwa kuwa  Mshindi wa Tuzo ya Mwanamke Kinara Uongozi wa Taasisi za Umma  Kanda ya Ziwa nafasi ambayo alikuwa anachuana na Khadija Mbarouk kutoka TANESCO, Nyanjige Petro kutoka MWAUWASA, Helga Mfuruki kutoka TAKUKURU Shinyanga na Bahati Mwaifuge ambaye ni Ofia Uhamiaji wa mkoa wa Mwanza.

Mratibu wa Tuzo za Mwanamke Kinara Kanda ya Ziwa, Khadija Liganga alisema tuzo hizo zitaongeza hamasa kwa wanawake kuongeza jitihada katika kutimiza wajibu wao kwenye nyanja mbalimbali.

Kwa mara ya tano kongamano la 'Women Round Table' limekuwa likifanyika jijini Mwanza ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani huku Tuzo za Mwanamke Kinara Kanda ya Ziwa kifanyika kwa mara ya kwanza mwaka huu 2021 kwa kuhusisha sekta 16.
Mratibu wa Tuzo za Mwanamke Kinara Kanda ya Ziwa, Khadija Liganga akizungumza  wakati wa utoaji tuzo za Mwanamke kinara Kanda ya Ziwa ambapo alisema tuzo hizo zitaongeza hamasa kwa wanawake kuongeza jitihada katika kutimiza wajibu wao kwenye nyanja mbalimbali.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha Tuzo ya Mwanamke Kinara Uongozi wa Taasisi za Umma Kanda ya Ziwa 2021 aliyopata.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akizungumza baada ya kupewa Tuzo ya Mwanamke Kinara Uongozi wa Taasisi za Umma Kanda ya Ziwa 2021. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Mwanamke Kinara Uongozi wa Taasisi za Umma Kanda ya Ziwa 2021 akionesha cheti cha ushiriki wa mashindano ya tuzo ya Mwanamke Kinara Kanda ya Ziwa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Mwanamke Kinara Uongozi wa Taasisi za Umma Kanda ya Ziwa 2021
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Mwanamke Kinara Uongozi wa Taasisi za Umma Kanda ya Ziwa 2021 akipiga picha ya kumbukumbu na wafanyakazi wenzake

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA YALIYOJIRI WAKATI WA KUTOA TUZO ZA MWANAMKE KINARA KANDA YA ZIWA 2021


PICHA NA BMG BLOG

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post