SHAMIMU NA MUMEWE KUHUKUMIWA JUMATANO


Mahakama  Kuu kitengo cha Uhujumu Uchumi na Makosa ya Rushwa, maarufu kama Mahakama ya Mafisadi iliyopo Jijini Dar es Salaam, imepanga kutoa hukumu dhidi ya mfanyabiashara, Abdul Nsembo (45) maarufu kama Abdulkandida na mkewe, Shamim Mwasha (41) Jumatano Machi 31, Mwaka huu.

Hukumu hiyo itatolewa baada ya upande wa mashtaka na wa utetezi kumaliza kutoa ushahidi wao.

Upande wa mashtaka ulipeleka mashahidi sita na vielelezo 8  huku upande wa utetezi ukuwa na mashahidi watatu.

Shamimu ambaye ni mmiliki wa Blog ya 8020 na mumewe Nsembo, wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroini gramu 439.70, wanadaiwa kutenda tukio hilo Mei mosi 2019 huko Mbezi Beach jijini Dar es Salaam. Kesi hiyo inasikilizwa na Jaji Elinaza Luvanda.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments