SERIKALI YATANGAZA TAHASUSI ‘COMBINATIONS’ MPYA KWA WANAFUNZI WATAKAOINGIA KIDATO CHA TANO 2021 | MALUNDE 1 BLOG

Monday, March 29, 2021

SERIKALI YATANGAZA TAHASUSI ‘COMBINATIONS’ MPYA KWA WANAFUNZI WATAKAOINGIA KIDATO CHA TANO 2021

  Malunde       Monday, March 29, 2021

Serikali imetangaza kuanza kwa tahasusi (Combination) mpya tano kwa ajili ya wanafunzi watakaoingia kidato cha tano mwaka 2021.

Lengo la kuongeza tahasusi hizo ni kuondoa changamoto ya ukosefu wa wataalam nchini ambayo imekuwepo kwa muda mrefu.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Seleman Jafo leo Jumatatu Machi 29, 2021 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Tahasusi hizo ni  Physics, Mathematics, Computer Studies (PMC); Kiswahili, French ,Chinese  (KFC); Kiswahili, English, Chinese (KEC); Physical Education, Biology, Fine Art (PBF) na Physical Education, Geography, Economics (PGE).

Jafo amesema tahsusi ya PMC itatolewa katika shule ya sekondari ya  Dodoma ambayo itakuwa maalumu kwa wasichana ambapo kwa wavulana itakuwa sekondari ya wavulana ya Iyunga.

Amesema tahsusi ya  KFC na KEC itatolewa katika shule ya sekondari ya wasichana Morogoro na ya wavulana Usagara wakati PBF na PGE  itatolewa shule ya sekondari ya wasichana ya Makambako, shule ya sekondari ya wavulana Kibiti na sekondari ya Mpwapwa ambayo ni ya mchanganyiko.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post