RC KUNENGE ATOA RATIBA NA UTARATIBU WA KUAGA MWILI WA MAGUFULI DAR ES SALAAMDk. John Pombe Magufuli 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge ametoa ratiba na utaratibu wa kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Marehemu Dkt. John Magufuli ambapo kwa Mkoa huo umepewa siku mbili za kutoa heshima za mwisho.

Akitoa ratiba hiyo RC Kunenge amesema Siku ya kesho Jumamos Machi 20 kuanzia saa 1:00 -3:00 Asubuhi itafanyika Misa takatifu kanisa Katoliki Mt. Petro, Saa 3:00 - 3:30 asubuhi Mwili wa Marehemu utawasili Uwanja wa Uhuru, Saa 3:30 - 4:30 asubuhi itafanyika Misa takatifu ambapo Saa 4:30 Asubuhi adi Saa 9: 30 Alasiri Viongozi wa Serikali, Vyama vya siasa, Wafanyakazi na Taasisi za umma watatoa heshima za mwisho na majira ya saa 9:30 - 12:00 Wananchi watatoa heshima za mwisho.

Aidha Kunenge amesema Siku ya Jumapili Saa 2:00 Asubuhi mwili wa Marehemu utawasili Uwanja wa Uhuru, Saa 2:30 Asubuhi adi Saa 10:30 Jioni Wananchi watatoa heshima za mwisho ambapo Saa 10:30 Jioni adi Saa 11:00 jioni Mwili utaelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ambapo saa 11:00 jioni adi Saa 11:45 jioni Mwili utasaririshwa kutoka Dar es salaam kuelekea Dodoma.

Katika hatua nyingine Kunenge ametoa kibali kwa Daladala, Bajaji na Bodaboda kupeleka wananchi Uwanja wa Uhuru atakama hawana route za ili kurahisisha suala la usafiri huku akitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi.

Pamoja na hayo Kunenge amepiga marufuku kufanyika kwa sherehe kwa siku zote 21 za maombolezo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post