Picha : DC MBONEKO AZINDUA RASMI MRADI WA MAJI SAFI MWAWAZA - NEGEZI....WIKI YA MAJI MKOA WA SHINYANGA


Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akifungua bomba la maji wakati akizindua Mradi wa Maji Safi Mwawaza – Negezi wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Maji Duniani Mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Machi 16,2021 katika kijiji cha Mwawaza kata ya Mwawaza Manispaa ya Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko amezindua rasmi Mradi wa Maji Safi Mwawaza – Negezi katika Manispaa ya Shinyanga uliogharimu shilingi Bilioni 1.4 kutoka serikali kuu kupitia Wizara ya Maji na Mfuko wa Maji unaotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) ukitarajiwa kunufaisha wakazi 15,429 wa vijiji vya Mwawaza na Negezi kata ya Mwawaza.

Mradi huo wa Maji kutoka Ziwa Victoria umezinduliwa leo Jumanne Machi 16,2021 na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Maji Duniani ambayo hufanyika kila ikifapo Machi 16 hadi Machi 22 kila mwaka.

Akitoa taarifa kuhusu mradi huo, Kaimu Mtendaji wa SHUWASA Mhandisi Yusuph Katopola amesema lengo kuu la mradi ni kufikisha huduma ya maji safi katika kata ya Mwawaza ambayo haikuwa na huduma ya maji safi kutoka SHUWASA ambapo wananchi walikuwa wanatumia maji yasiyo safi na yasiyotosheleza kutoka kwenye visima vifupi.

“Ujenzi wa mradi huu ulianza Mwezi Februari mwaka 2020 na unatarajiwa kukamilika mwezi Machi 2021 ambapo chanzo cha maji ni Ziwa Victoria . SHUWASA inanunua maji kutoka KASHWASA ambaye ni muuzaji wa maji ya jumla. Kukamilika kwa mradi huu kutaboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi kwa wakazi wote wa kata ya Mwawaza na vijiji vya jirani”,ameeleza Mhandisi Katopola.

Amesema hadi Machi 15,2021 ujenzi umekamilika kwa asilimia 98 akizitaja shughuli zilizokamilika kuwa ni pamoja na ujenzi wa matenki ya kuhifadhia maji,ulazaji mabomba,ujenzi wa vituo vya kuchotea maji,uungaji wa umeme kwenye kituo cha kusukuma,ufungaji pampu na ukarabati wa nyumba ya mtumishi na nyumba ya pampu ambao umekamilika kwa asilimia 95 ambapo kazi iliyobaki ni kujenga chemba mbalimbali kwenye mtandao wa maji wa usafirishaji na usambazaji.

Akizungumza wa uzinduzi wa Mradi wa Maji Safi Mwawaza – Negezi, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kusikia kilio cha wananchi wa Mwawaza ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya maji.

“Tunawashukuru SHUWASA kwa kusimamia vizuri ujenzi wa mradi huu wa maji ambao unaondoa adha ya maji. ambapo akina mama ndiyo walikuwa wanapata tabu zaidi wakitumia muda mwingi kutafuta maji. Leo tunawatua ndoo kichwani wanawake wa Mwawaza na tutahakikisha vijiji jirani pia vinapata huduma ya maji safi”,amesema Mboneko.

“Ninaziomba Mamlaka zote zinazohusika na masuala ya Maji ikiwemo SHUWASA, RUWASA,KUWASA na KASHWASA kuhakikisha wanasimamia ipasavyo miradi ya maji kwani wananchi wanataka maji badala ya maneno . Fikisheni huduma ya maji kwenye maeneo ambayo hayana maji ikiwemo kwenye taasisi”,ameongeza Mboneko.

“Uwepo wa maji unachangia maendeleo kwa sababu wananchi wataanzisha shughuli mbalimbali. Tuendelee kuiamini serikali kwa maendeleo tunayoendelea kupata kwani maendeleo yanakuja hatua kwa hatua. Kama inavyosema Kauli mbiu ya Wiki ya Maji Duniani mwaka huu 'Thamani ya maji kwa uhai na maendeleo', naomba mtunze vyanzo vya maji kwani maji ni uhai", amesema.

Aidha Mkuu huyo wa wilaya amewapongeza wananchi kwa ushirikiano wanaoendelea kuuonesha katika utekelezaji wa miradi ya maji huku akiwataka wasimamizi wa vituo vya kutolea maji wawepo muda wote ili wananchi wapate huduma ya maji.

 Kwa upande wake, Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga, Lucy Enock ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa vitendo huku akiwataka wananchi kulinda miundo mbinu ya maji ili idumu kwa muda mrefu.

Diwani wa kata ya Mwawaza, Juma Nkwabi na Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi bwana Samwel Jackson wameshukuru kutekelezwa kwa mradi huo wa maji hali itakayosaidia wananchi kuondokana na adha ya maji.

Kwa upande wao wakazi wa Mwawaza wameeleza kupokea kwa furaha mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria wakisema walikuwa na changamoto ya maji kwa muda mrefu hali iliyokuwa inasababisha wakati mwingine ndoa kujawa na migogoro kutokana na wanawake kutumia muda mwingi kusaka maji hadi nyakati za usiku.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akizindua Mradi wa Maji Safi Mwawaza – Negezi katika Manispaa ya Shinyanga uliogharimu shilingi Bilioni 1.4  wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Maji Duniani Mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Machi 16,2021 katika kijiji cha Mwawaza kata ya Mwawaza Manispaa ya Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kaimu Mkurugenzi wa SHUWASA, Mhandisi Yusuph Katopola akisoma taarifa ya ujenzi wa Mradi wa Maji Safi Mwawaza – Negezi katika Manispaa ya Shinyanga uliogharimu shilingi Bilioni 1.4 wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Maji Duniani Mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Machi 16,2021 katika kijiji cha Mwawaza kata ya Mwawaza Manispaa ya Shinyanga. 
Kaimu Mkurugenzi wa SHUWASA, Mhandisi Yusuph Katopola (kushoto)  akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko taarifa ya  Mradi wa Maji Safi Mwawaza – Negezi katika Manispaa ya Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya kuchotea maji katika kijiji cha Mwawaza kwenye Mradi wa Maji Safi Mwawaza – Negezi katika Manispaa ya Shinyanga ambapo shughuli ya uzinduzi wa mradi huo imefanyika wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Maji Duniani Mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Machi 16,2021.
Muonekano wa sehemu ya kuchotea maji katika kijiji cha Mwawaza kwenye Mradi wa Maji Safi Mwawaza – Negezi katika Manispaa ya Shinyanga ambapo shughuli ya uzinduzi wa mradi huo imefanyika wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Maji Duniani Mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Machi 16,2021.
Muonekano wa sehemu ya kuchotea maji katika kijiji cha Mwawaza kwenye Mradi wa Maji Safi Mwawaza – Negezi katika Manispaa ya Shinyanga ambapo shughuli ya uzinduzi wa mradi huo imefanyika wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Maji Duniani Mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Machi 16,2021.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Maji Safi Mwawaza – Negezi katika Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizindua Mradi wa Maji Safi Mwawaza – Negezi katika Manispaa ya Shinyanga uliogharimu shilingi Bilioni 1.4  wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Maji Duniani Mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Machi 16,2021 katika kijiji cha Mwawaza kata ya Mwawaza Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati akizindua Mradi wa Maji Safi Mwawaza – Negezi katika Manispaa ya Shinyanga uliogharimu shilingi Bilioni 1.4  wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Maji Duniani Mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Machi 16,2021 katika kijiji cha Mwawaza kata ya Mwawaza Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akifungua bomba la maji wakati akizindua Mradi wa Maji Safi Mwawaza – Negezi wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Maji Duniani Mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Machi 16,2021 katika kijiji cha Mwawaza kata ya Mwawaza Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akifungua bomba la maji wakati akizindua Mradi wa Maji Safi Mwawaza – Negezi wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Maji Duniani Mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Machi 16,2021 katika kijiji cha Mwawaza kata ya Mwawaza Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiangalia maji yanavyotoka wakati akizindua Mradi wa Maji Safi Mwawaza – Negezi wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Maji Duniani Mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Machi 16,2021 katika kijiji cha Mwawaza kata ya Mwawaza Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati akizindua Mradi wa Maji Safi Mwawaza – Negezi wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Maji Duniani Mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Machi 16,2021 katika kijiji cha Mwawaza kata ya Mwawaza Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) akimtwisha kichwani ndoo ya maji mmoja wa wanawake wakati akizindua Mradi wa Maji Safi Mwawaza – Negezi wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Maji Duniani Mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Machi 16, 2021 katika kijiji cha Mwawaza kata ya Mwawaza Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kulia) akimtwisha kichwani ndoo ya maji mmoja wa wanawake wakati akizindua Mradi wa Maji Safi Mwawaza – Negezi wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Maji Duniani Mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Machi 16, 2021 katika kijiji cha Mwawaza kata ya Mwawaza Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (katikati) akizungumza baada ya kuwatwisha kichwani ndoo za maji akina mama wakati akizindua Mradi wa Maji Safi Mwawaza – Negezi wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Maji Duniani Mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Machi 16, 2021 katika kijiji cha Mwawaza kata ya Mwawaza Manispaa ya Shinyanga.
Mkazi wa Mwawaza Mwatano Salum akiishukuru serikali kupeleka maji Mwawaza.
Mkazi wa Mwawaza Lucas Kulwa akiishukuru serikali kwa kupeleka maji katika kata ya Mwawaza
Katibu wa Siasa na Uenezi kata ya Mwawaza Bi. Zainab Lugaila akiishukuru serikali kutekeleza kwa vitendo ahadi ya kupeleka maji Mwawaza
Diwani wa kata ya Mwawaza, Juma Nkwabi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Maji Safi Mwawaza – Negezi.
Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga Lucy Enock akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Maji Safi Mwawaza – Negezi.
Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM wilaya ya Shinyanga Saidi Bwanga akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Maji Safi Mwawaza – Negezi 
Mwenyekiti wa kijiji cha Mwawaza kata ya Mwawaza, Juma Kalima Nyanda akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Maji Safi Mwawaza – Negezi 
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (Patrobas Katambi) , Samwel Jackson akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Maji Safi Mwawaza – Negezi 
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, John Tesha akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Maji Safi Mwawaza – Negezi 
Mwenyekiti wa CCM kata ya Mwawaza, Shija John akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Maji Safi Mwawaza – Negezi 
Wananchi wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Maji Safi Mwawaza – Negezi 
Meneja wa RUWASA mkoa wa Shinyanga Julieth Payovela akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Maji Safi Mwawaza – Negezi 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SHUWASA, Mwamvua Jilumbi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Maji Safi Mwawaza – Negezi 
Wananchi wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Maji Safi Mwawaza – Negezi 
Wananchi wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Maji Safi Mwawaza – Negezi.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post