WATENDAJI WIZARA YA MALIASILI WAKAGUA VIJIJI VILIVYOVAMIWA NA TEMBO ENEO LA USHOROBA MAKUYUNI ARUSHA

Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Mhe. ACP Edward Balele akizungumza na baadhi ya watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii na wataalam kutoka TAWA, TANAPA na TAWIRI kuhusu namna ya kutatua changamoto ya uvamizi wa tembo kwenye eneo la ushorobo la vijiji vya Makuyuni, Wilayani Monduli katika kikao kilichofanyika leo kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Monduli.
Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Mhe. ACP Edward Balele (katikati mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii na wataalam kutoka TAWA, TANAPA na TAWIRI baada ya kikao kilichozungumzia namna ya kutatua changamoto ya uvamizi wa tembo kwenye eneo la ushorobo la vijiji vya Makuyuni, Wilayani Monduli kilichofanyika leo kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Monduli.
Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Mhe. ACP Edward Balele (katikati) akiteta jambo na Afisa Wanyamapori Mkuu, Pellage Kauzeni (kulia) ambaye pia ni Kiongozi wa Msafara kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii mara baada ya kikao kilichohusu namna ya kutatua changamoto ya uvamizi wa tembo kwenye eneo la ushorobo la vijiji vya Makuyuni, Wilayani Monduli kilichofanyika leo kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Monduli. Kushoto ni Afisa Wanyamapori Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii , Antonia Raphael.
Baadhi ya watendaji kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii wakiongozwa Afisa Wanyamapori Mkuu, Pellage Kauzeni (kushoto) na wataalam kutoka TAWA, TANAPA na TAWIRI, wakikagua moja ya shamba lililovamiwa na tembo katika kitongoji cha Lemioni, Makuyuni Wilaya ya Monduli leo.
Afisa Wanyamapori Mkuu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Silvanus Okudo akionyesha namna tembo alivyofanya uharibifu katika kijiji cha Naiti, Makuyuni, Wilaya ya Monduli leo. Wanaoshuhudia ni Afisa Wanyamapori Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii , Antonia Raphael (wa pili kutoka kulia) na Mtafiti Mwandamizi kutoka TAWIRI, Hamza Kija (kushoto).
Mtafiti Mwandamizi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Chediel Mrisha akiteta jambo na Mtafiti Mwandamizi kutoka TAWIRI, Hamza Kija (kushoto) katika ziara ya kikazi ya kukagua maeneo yaliyovamiwa na tembo yaliyoko Makuyuni, Wilaya ya Monduli.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments