MBUNGE NEEMA LUGANGIRA: ASASI ZA KIRAIA (NGOs) NCHINI ZITAMPA USHIRIKIANO MKUBWA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia Kundi la Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Mh Neema Lugangira akizungumza Bungeni Jijini Dodoma leo wakati wa kuchangia kwenye Maazimio Mawili; Kumuenzi Hayati Rais Magufuli na Kumpongeza Mhe Rais Samia
MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia Kundi la Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Mh Neema Lugangira Bungeni Jijini Dodoma wakati wa kuchangia kwenye Maazimio Mawili; Kumuenzi Hayati Rais Magufuli na Kumpongeza Mhe Rais Samia

NA MWANDISHI WETU, DODOMA.

MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia Kundi la Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Mh Neema Lugangira amesema Asasi za Kiraia (CSOs na NGOs) hapa nchini zitampa ushirikiano mkubwa Mhe Rais Samia Suluhu Hassan katika kutekeleza Dira na mipango yake ya maendeleo ya Taifa la Tanzania.

Mh Neema Lugangira ameyasema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma wakati wa kuchangia kwenye Maazimio Mawili; Kumuenzi Hayati Rais Magufuli na Kumpongeza Mhe Rais Samia ambapo pia alisema kwamba wiki hii Asasi zaidi ya 200 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar zimewasilisha tamko la pole na salamu za Pongezi kwa Mhe Rais Samia Suluhu Hassani ikiwemo Jukwaa la Wanawake Wakurugenzi wa Asasi za Kiraia (CSOs na NGOs) nao wametoa tamko la pongezi kwa Rais.

Alisema kwamba Sekta ya Asasi za Kiraia ina imani kubwa sana naye kwa sababu anauzoefu mkubwa sana wa uongozi na mafanikio lukuki ambayo yatawezsha kuleta tija kubwa kwa maendeleo ya Taifa letu la Tanzania

“Lakini nitumie fursa hii kutaja maeneo machache: Mhe Rais Samia Suluhu Hassan alianza ajira yake kwenye mwamvuli mashirika yasiyokwa ya kuserikali linaloitwa ANGOZA (Association for Non Governmental Organisations in Zanzibar) hivyo ni mwana Azaki mwezetu na ana uzoefu mkubwa ambao utakuwa chachu kwetu”Alisema

Mbunge Neema alisema Rais Samia anauzoefu mkubwa sana kwenye masuala ya uwezeshwaji kiuchumi na kupitia uzoefu huo mwaka 2016 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon alimteua Rais Samia akiwa Makamu wa Rais kuwa Mjumbe wa Jopo la Dunia kama Mwakilishi wa Afrika la kumshauri namna bora ya kufanikisha Uwezeshwaji Wanawake Kiuchumi.

Alisema la tatu ni kwamba miaka 25 iliyopita Rais Samia akiwa anatokea kwenye NGOs alishiriki kwenye Mkutano wa Beijing uliokuwa unalenga kuleta ukombozi wa usawa na kijinsia ikiwemo wanawake kwenye nafasi za uongozi na maamuzi.

Aidha alisema kupitia yeye kuwa Rais wa kwanza Mwanamke wa Tanzania ameiwezesha Tanzania kuweka historia ya kuwa sehemu ya Utekelezaji wa Maazimio ya Beijing 

Mbunge Neema aliongezea kuwa akiwa kama mdau wa lishe wao wanatambua kuwa juhudi kubwa ambazo Mhe Rais Samia ameweka katika kuhakikisha Serikali inaboresha hali ya lishe hapa nchini.

Mbunge huyo alisema vivyo hivyo wanatambua jitihadi kubwa za Makamu wa Rais Mteule, Mhe Dkt Philip Mpango ameweka kwenye kuboresha hali ya lishe kwa kuhakikisha kwamba Halmashauri zinatenga bajeti ya lishe kwa kulingana na idadi ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

“Mh Naibu Spika napenda kuwasilisha ombi rasmi kwa Mhe Rais Samia Suluhu Hassan la kukutana na Sekta ya Asasi za Kiraia  ili nasi pia tuwe sehemu ya mafanikio yake”,alisema Mbunge Neema Lugangira

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments