RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI WA WENYEVITI NA KATIBU | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, March 30, 2021

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI WA WENYEVITI NA KATIBU

  Malunde       Tuesday, March 30, 2021


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Florencs Turuka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Utumishi wa Umma akichukua nafasi ya Dkt. Charles Msonde ambaye amemaliza muda wake.

Rais Samia pia amemteua Mhandisi Dkt. Richard Masika kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) akichukua nafasi ya Prof. Patrick Makungu ambaye muda wake umekwisha, mwingine aliyeteuliwa ni Dkt. Blandina Lugendo ambaye anakuwa Mwenyekiti wa Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) .

Rais Samia pia amemteua Paulina Nkwama kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu, kabla ya uteuzi Nkwama alikuwa Katibu Tawala Msaidizi (Elimu) Mkoa wa Kilimanjaro na anachukua nafasi ya Winfrida Rutaindurwa ambaye amemaliza muda wake.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post