MAELFU YA WANANCHI DAR WAJIPANGA BARABARANI MWILI WA JPM UKIPITISHWA.....VILIO VYATAWALA KILA KONA


Wananchi wa eneo la Kinondoni B na Biafra wakiwa kandokando ya barabara kwaajili ya kuaga mwili wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli leo Machi 20, 2021.
Na Said Mwishehe,Michuzi TV
MAELFU ya wananchi wa Mkoa Dar es Salaam wamejitokeza kwa wingi kwenye barabara ambayo mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli unapitishwa ukitokea Kanisa la St.Peters kuelekea Uwanja wa Uhuru.

Wananchi hao walianza kujitokeza mapema ya alfajiri katika barabara ya Moroco,Magomeni,Ilala Boma,Chang'ombe , Chuo Kikuu cha Ualimu Dar es Salaam( DUCE) hadi Uwanja wa Uhuru.

Barabarani watu waliokuwa wamejazana kushuhudia jeneza la mpendwa wetu Dk. Magufuli,wengi wao walishindwa kujizua.  Wakijikuta wakiangaua vilio ,wengine wakionekana wako chini kutokana na kuishiwa nguvu.

Hakika ni majonzi na simanzi kubwa iliyokuwa imetawala .Mwili wa Dk.Magufuli ulianza kupitishwa barabarani kuanzia saa tatu baada ya kumalzika kwa ibada maalum iliyofanyika Kanisa la St.Peters mkoani Dar es Salaam.

Kadri mwili ulivyokuwa unapita barabarani ndivyo ambavyo idadi ya wananchi ilivyokuwa ikiongezeka ili kushuhudia mwili wa Dk.Magufuli ukpitishwa.Wananchi waliokuwa barabarani mbali ya kuangua vilio na kujawa na simanzi , wengine walikuwa wameshika majani ya matawi ya miti

UPDATES ZOTE

Pakua / Download App ya Malunde 1 blog Tuwe tunakutumia taarifa zote moja kwa moja kwenye simu yako bure kabisa 

Bofya <<HAPA>> Mara Moja TuDownload/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post