EZIMINA ALLY ASAINI KITABU CHA KUMBUKUMBU YA MAOMBOLEZO KIFO CHA JPM

Mkazi wa Shinyanga Ezimina Ally ambaye ni Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni inayotengeneza vinywaji baridi , SBC Tanzania Limited (Pepsi) Shinyanga, akitia saini Kitabu cha Kumbukumbu ya Maombolezo kufuatia Kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Jumamosi Machi 20,2021 katika ofisi ya Mkuu wa  Mkoa wa Shinyanga
**
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkazi wa Shinyanga Ezimina Ally ambaye ni Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni inayotengeneza vinywaji baridi , SBC Tanzania Limited (Pepsi) Shinyanga, ametoa pole kwa mjane wa aliyekuwa Rais wa Tanzania awamu ya tano, Dkt. John Pombe Magufuli, Mama Janeth Magufuli, wana familia, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote wakiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Ezimina Ally ametoa pole hizo leo Jumamosi Machi 20,2021 wakati akitia Saini Kitabu cha Kumbukumbu ya Maombolezo kufuatia Kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika eneo maalumu lililotengwa na Serikali ya Mkoa wa Shinyanga katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya Viongozi na Wananchi kutoa pole na salamu za rambirambi.

Ezimina Ally ambaye Mwaka 2020 alitia nia kugombea Ubunge Jimbo la Muleba Kusini mkoani Kagera amesema Dk. Magufuli alikuwa Mcha Mungu, mtu wa watu na mtetezi wa wanyonge.

“Tumepoteza Shujaa katika taifa letu na katika Bara la Afrika kwa ujumla. Tutamkumbuka Magufuli kwa utawala wake kwani ameacha alama kubwa katika taifa letu akipigania maendeleo ya nchi. Kifo chake kimetuacha na Sintofahamu kuwa kesho yetu itakuwaje”,amesema Ezimina.

Katika hatua nyingine, Ezimina amesema ana imani kubwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ni mpambanaji hivyo ataweza kuliongoza vizuri taifa la Tanzania na kwamba ni vyema kumuombea aweze kusimama imara na kuliongoza taifa kwa weledi na hatimaye kutuvusha salama.

Mkurugenzi wa Kambesha Insurance Agency, Bertha Kambesha amesema atamkumbuka Dkt. Magufuli kwa namna alivyopigania haki za Wanyonge na mara kwa mara aliwasisitiza Watanzania wasimuache Mungu.

"Magufuli alikuwa Mcha Mungu, mpenda watu. Tulipewa zawadi na Mungu na Magufuli amekamilisha kufanya kazi alizopewa na Mungu naomba tuendeleze yote aliyoyaanzisha",amesema Kambesha.
Mkazi wa Shinyanga Ezimina Ally ambaye ni Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni inayotengeneza vinywaji baridi , SBC Tanzania Limited (Pepsi) Shinyanga, akiwasili katika eneo maalumu lililotengwa na Serikali ya Mkoa wa Shinyanga katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya Viongozi na Wananchi kutoa pole na salamu za rambirambi ili atie saini Kitabu cha Kumbukumbu ya Maombolezo kufuatia Kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Jumamosi Machi 20,2021
Mkazi wa Shinyanga Ezimina Ally ambaye ni Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni inayotengeneza vinywaji baridi , SBC Tanzania Limited (Pepsi) Shinyanga, akiwasili katika eneo maalumu lililotengwa na Serikali ya Mkoa wa Shinyanga katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya Viongozi na Wananchi kutoa pole na salamu za rambirambi ili atie saini Kitabu cha Kumbukumbu ya Maombolezo kufuatia Kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Jumamosi Machi 20,2021
Mkazi wa Shinyanga Ezimina Ally ambaye ni Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni inayotengeneza vinywaji baridi , SBC Tanzania Limited (Pepsi) Shinyanga, akitia saini Kitabu cha Kumbukumbu ya Maombolezo kufuatia Kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Jumamosi Machi 20,2021 katika ofisi ya Mkuu wa  Mkoa wa Shinyanga
Mkazi wa Shinyanga Ezimina Ally ambaye ni Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni inayotengeneza vinywaji baridi , SBC Tanzania Limited (Pepsi) Shinyanga, akitafakari wakati akitia saini Kitabu cha Kumbukumbu ya Maombolezo kufuatia Kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Jumamosi Machi 20,2021 katika ofisi ya Mkuu wa  Mkoa wa Shinyanga
Mkurugenzi wa Kambesha Insurance Agency, Bertha Kambesha akitia saini Kitabu cha Kumbukumbu ya Maombolezo kufuatia Kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Jumamosi Machi 20,2021 katika ofisi ya Mkuu wa  Mkoa wa Shinyanga
Mkurugenzi wa Kambesha Insurance Agency, Bertha Kambesha akitia saini Kitabu cha Kumbukumbu ya Maombolezo kufuatia Kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Jumamosi Machi 20,2021 katika ofisi ya Mkuu wa  Mkoa wa Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

UPDATES ZOTE

Pakua / Download App ya Malunde 1 blog Tuwe tunakutumia taarifa zote moja kwa moja kwenye simu yako bure kabisa 

Bofya <<HAPA>> Mara Moja TuDownload/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post