Picha : MWILI WA HAYATI DK. MAGUFULI ULIVYOWASILI UWANJA UHURU...VILIO NA SIMANZI VYATAWALA


Mwili wa Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dk. John Pombe Magufuli ukiwasili kwenye uwanja wa Uhuru kwa ajili ya ibada maalum na viongozi pamoja na wananchi wa mkoa wa Dar es salaam kuaga. (PICHA NA JOHN BUKUKU -DAR ES SALAAM)
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kuwaongoza watanzania katika ibada maalum ya kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dk. John Pombe Magufuli, Shughuli za kuaga mwili zitafanyika kuanzia leo mpaka kesho ambapo viongozi mbalimbali watashiriki kuaga pamoja na wananchi wa mkoa wa Dar es salaam.
Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wakiwa tayari kupokea mwili wa Hayati Dk. John Pombe Magufuli kwenye uwanja wa Uhuru.
Mwili wa Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dk. John Pombe Magufuli ukiwasili kwenye gari maalum la kijeshi kwenye uwanja wa Uhuru kwa ajili ya ibada maalum na viongozi pamoja na wananchi wa mkoa wa Dar es salaam kuaga.
Viongozi mbalimbali wakiingia kwenye uwanja wa Uhuru wakati wmili wa Hayati Dk. John Pombe Magufuli ulipowasili kwa ajili ya ibada.
Mwili wa Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dk. John Pombe Magufuli ukitolewa kwenye kanisa la Saint Peter Oysterbay kuelekea uwanja wa Uhuru kwa ajili ya ibada maalum na viongozi pamoja na wananchi wa mkoa wa Dar es salaam kuaga.
Baadhi ya wasaidizi wa hayati Dk. John Pombe Magufuli wakiingia kwenye uwanja wa uhuru kwa ajili ya kushiriki ibada hiyo.
Picha mbalimbali zikionesha hali ya simanzi na majozi ilivyokuwa wakati mwili wa hayati Rais Dk. John Pombe Magufuli akipita katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam kwenda uwanja wa Uhuru ambako ibada maalum ya kuaga mwili inafanyika.
UPDATES ZOTE

Pakua / Download App ya Malunde 1 blog Tuwe tunakutumia taarifa zote moja kwa moja kwenye simu yako bure kabisa 

Bofya <<HAPA>> Mara Moja Tu


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post