JAMAA AFUNGA NDOA NA WAREMBO WAWILI SIKU MOJA...ASEMA AMETIMIZA NDOTO YAKE YA UTOTONI


Adamu akiwa na wake zake aliowaoa siku moja
Babangida Sadiq Adamu, ambaye ni kiongozi wa chama cha vijana All Progressives Congress (APC), amezua mjadala moto mtandaoni baada ya kufunga pingu za maisha na wake wawili siku moja jijini Abuja nchini Nigeria.

Adamu alifanya harusi Jumamosi Machi 6, 2021 mjini Abuja na wapenzi wake Malama Maimuna Mahmud na Malama Maryam Muhammad Na'ibi.

Harusi ya kwanza Fatiha, iliandaliwa katika Msikiti ya Kado Bmiko Juma mkabala na Shule ya Msingi ya Kado Bmiko Primary, 1st Avenue Gwarinpa saa nne asubuhi na ya pili iliandaliwa katika Msikiti wa Garki Village Central, Garki II Abuja mwendo wa saa saba mchana.

Akizungumzia kuhusu sababu za kuwaoa wake wawili siku moja, Adamu ambaye anaripotiwa kujihusisha na Biashara ya mali isiyohamishika, alisema ilikuwa ndoto yake tangu utotoni kuoa wake wawili siku moja.

"Kwa muda mrefu imekuwa ndoto yangu kuoa wake wawili siku moja, baadhi ya watu walihisi kwamba haiwezakani lakini amewezesha itendeke," alisema.

Wanamtandao wengi walimtakia Adamu heri njema katika ndoa yake wengine wakiibua hisia mseto.

Preyer Pieces: "Tafadhali mbona wanawake wasiolewe na waume wawili pia? Endapo unaolewa na waume wawili unabadilisha nyumba ukichoka kukaa na mmoja."

James Gabriel: "Hongera kaka. Mungu akupe nyumba iliyojaa furaha na baraka zaidi"

Gozzy: "Hongera mkubwa. Nakuombea uwe na amani"

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments