MARUFUKU WATOTO WA KIKE KUOSHWA DAWA YA MVUTO WA MAPENZI ‘SAMBA’


Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Msalala Neema Katengesya akizungumza wakati wa mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa watu maarufu katika kata ya Lunguya kwa lengo la kujenga uelewa wa jamii kuhusu mila na desturi zinazochangia ukatili wa kijinsia
****
Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, Mkoani Shinyanga imepiga marufuku wananchi na waganga wa kienyeji kuwaosha watoto wa kike ‘wanafunzi’ dawa za mvuto wa mapenzi maarufu kama samba ili kutomokeza mimba na ndoa za utotoni katika halmashauri hiyo.

Akizungumza jana Machi 25,2021 wakati wa mdadalo wa jamii ulioandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikina na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya watu (UNFPA) Afisa Maendeleo ya Jamii wilaya ya Msalala, Bi. Neema Katengisya alisema kwamba, ni marufuku kwa wazazi kuwapeleka wasichana wenye umri chini ya miaka 18 walioko shuleni au nje ya shule kwa waganga wa kienyeji kwani vitendo hivyo vinachochoea wasichana kujiingiza kwenye mahusiano ya mapenzi kabla ya wakati.

Mdahalo huo, ulioandaliwa na TGNP kwa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia umewakutanisha zaidi ya watu 300 wenye ushawishi kwa jamii katika kata ya Lunguya na Shilela Halmashauri ya wilaya ya Msalala.

“Vitendo vyoyote vinavyojenga mazingira ya kuchochoa wasichana wa shule kujiingiza kwenye mahusiano ya kingono au ndoa za utotoni ni kosa kisheria, ninawataka waganga na wazee wa mila mliopo hapa, msiwapokee kabisa wasichana wadogo ambao wana umri chini ya miaka 18 kuwapa dawa za mvuto, wazazi ninawataka mbadilike, muache tabia hizo kwa sababu zinawapotezea watoto ndoto zao za maisha hasa ya kupata elimu”,alisema na Neema na kuongeza:

“..Tutaondoka katika hali hii endapo kila mmoja atakuwa tayari kubadilika na kuwa na mitazamo chanya kuhusu wanawake na watoto kama vile kutokubali watoto waolewe katika umri mdogo, wazee wa mila maarufu ‘Wakango’ kuepuka kukaa uchi na kutumia lugha chafu wakati wa sherehe wanazoandaa kuhusu watoto mapacha”,alisema.

Mdahalo huo ambao umefanyika Machi 25,2021 kwa lengo la kujenga uelewa wa jamii kuhusu mila na desturi zinazochangia ukatili wa kijinsia na kubadilisha mtazamo ili kutokomeza ukatili wa kijinsia na kushiriki katika shughuli za maendeleo.

Mwezeshaji kutoka TGNP, Deogratius Temba amesema mdahalo huo ni sehemu ya utekelezaji wa shughuli za mradi wa kubadili mtazamo hasi, mila na desturi zinazochangia uwepo wa ukatili wa kijinsia unaotekelezwa na TGNP na UNFPA katika kata ya Lunguya na Shilela halmashauri ya wilaya ya Msalala, mkoani Shinyanga.

Amesema TGNP inaendelea kushirikiana na serikali katika kutekeleza Mpango Mkakati wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) ikiwa imejikita zaidi katika kutokomeza mila, desturi na mitazamo zinazochochea ukatili wa kijinsia.

“Tumewakutanisha pamoja watu maarufu wenye ushawishi katika jamii katika kata ya Lunguya wakiwemo viongozi wa jeshi la jadi sungusungu,wazee wa mila (Wakango),viongozi wa dini,siasa,wafanyabiashara, wakulima, viongozi wa vitongoji, vijiji,wahudumu wa afya ngazi ya jamii na vituo vya taarifa na maarifa. Kwa upande wa kata ya Shilela tumefanya mdahalo na kundi la wanaume wenye miaka kuanzia 18 hadi 60 wanaotoka katika vikundi mbalimbali tofauti”, alifafanua Temba.

“Kupitia midahalo hii tunaamini kabisa italeta mabadiliko makubwa katika kutokomeza ukatili wa kijinsia, makundi haya ya wanaume yana nguvu na ushawishi lakini pia kuamsha ari ya wananchi kushiriki katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kama vile ujenzi wa zanahati ,vyoo na mabweni katika shule”,alisema Temba.

Wakizungumza wakati wa midahalo hiyo, washiriki walisema bado katika kata hizo kuna changamoto ya mimba na ndoa za utotoni, vipigo kwa wanawake, wanawake kutomiliki ardhi na kutoshirikishwa katika maamuzi, matumizi ya lugha mbaya (matusi) kwa wacheza ngoma ya ukango na wazazi kutokuwa karibu na watoto wao.

Wamesema hali duni ya kiuchumi na utandawazi na kukosekana kwa ulinzi kwa watoto vinachochea matukio ya ukatili wa kijinsia.

Kufuatia midahalo hiyo,wametengeneza mpango kazi kuhusu namna ya kutokomeza ukatili wa kijinsia katika maeneo yao huku wakipendekeza serikali za vijiji ziunde sheria ndogo kwa ajili ya kutokomeza ukatili wa kijinsia.

Diwani wa kaya ya Lunguya, Benedicto Mussa, aliwaasa viongozi wa vijiji vyote vitano vya kata hiyo kusimamia utekelezaji wa mpango kazi uliotengenezwa na washiriki wa mdahalo huo ili kuwa na tija na kuhakikisha vitendo vya Ukatili wa Kijinsia vinakoma kabisa katia kata hiyo hasa mila potofu na kandamizi ambazo zinachangia kurudisha maendeleo nyuma.

“Nyie mliopo hapa, kimsingi ndio watu ambao tuliwataka mje kwa sababu mna ushawishi na nguvu kayika jamii mnayoishi nayo, hatutarajii hali hii iendelee, tuna matumani makubwa ya kuona mabdiliko. Wenyeviti wa vijiji, huu mpango kazi tutautumia kuulizana kila tunapokutana kwenye vikao juu ya utekelezaji wake… baada ya mdahalo huu ndio kazi inaanza, hakuna kurudi nyuma…” alisema Mussa.
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Msalala Neema Katengesya akizungumza wakati wa mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa watu maarufu katika kata ya Lunguya kwa lengo la kujenga uelewa wa jamii kuhusu mila na desturi zinazochangia ukatili wa kijinsia. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Msalala Neema Katengesya akizungumza wakati wa mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa watu maarufu katika kata ya Lunguya kwa lengo la kujenga uelewa wa jamii kuhusu mila na desturi zinazochangia ukatili wa kijinsia
Diwani wa kata ya Lunguya Mhe. Benedict Mussa akizungumza wakati wa mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa watu maarufu katika kata ya Lunguya kwa lengo la kujenga uelewa wa jamii kuhusu mila na desturi zinazochangia ukatili wa kijinsia
Diwani wa kata ya Lunguya Mhe. Benedict Mussa akizungumza wakati wa mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa watu maarufu katika kata ya Lunguya kwa lengo la kujenga uelewa wa jamii kuhusu mila na desturi zinazochangia ukatili wa kijinsia
Mwezeshaji kutoka TGNP, Deogratius Temba akizungumza wakati wa mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa watu maarufu katika kata ya Lunguya kwa lengo la kujenga uelewa wa jamii kuhusu mila na desturi zinazochangia ukatili wa kijinsia
Mwezeshaji kutoka TGNP, Deogratius Temba akizungumza wakati wa mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa watu maarufu katika kata ya Lunguya kwa lengo la kujenga uelewa wa jamii kuhusu mila na desturi zinazochangia ukatili wa kijinsia
Mwezeshaji kutoka TGNP, Deogratius Temba akizungumza wakati wa mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa watu maarufu katika kata ya Lunguya kwa lengo la kujenga uelewa wa jamii kuhusu mila na desturi zinazochangia ukatili wa kijinsia
Mwezeshaji kutoka TGNP, Deogratius Temba akizungumza wakati wa mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa watu maarufu katika kata ya Lunguya kwa lengo la kujenga uelewa wa jamii kuhusu mila na desturi zinazochangia ukatili wa kijinsia
Watu maarufu kata ya Lunguya wakiendelea na mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia chini ya mti wa mwembe katika Senta ya Lunguya
Mshauri Jamii na Mtafiti kutoka TGNP, Catherine Mzurikwao akizungumza wakati wa mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa watu maarufu katika kata ya Lunguya kwa lengo la kujenga uelewa wa jamii kuhusu mila na desturi zinazochangia ukatili wa kijinsia
Mdahalo unaendelea
Mdahalo ukiendelea
Watu Maarufu kutoka Lunguya wakiwa kwenye mdahalo
Mganga wa Kienyeji Masanja Tabo akichangia hoja wakati wa mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia katika kata ya Lunguya
Mzee maarufu Helena Busobe akichangia hoja wakati wa mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia katika kata ya Lunguya
Mwana kituo cha taarifa na maarifa Lunguya, Gaudensia Madaha akichangia hoja wakati wa mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia katika kata ya Lunguya
Mdahalo ukiendelea
Kiongozi wa dini akichangia hoja wakati wa mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia katika kata ya Lunguya
Mdahalo ukiendelea
Mdahalo ukiendelea
Mdahalo ukiendelea
Kiongozi wa dini akichangia hoja wakati wa mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia katika kata ya Lunguya
Mzee Joseph Sonda akichangia hoja wakati wa mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia katika kata ya Lunguya
Mwenyekiti wa kituo cha taarifa na maarifa kata ya Lunguya Loyce Kabanza akichangia hoja wakati wa mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia katika kata ya Lunguya
Mdahalo ukiendelea
Mkazi wa Lunguya akichangia hoja wakati wa mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia katika kata ya Lunguya
Mdahalo unaendelea
Mshauri Jamii na Mtafiti kutoka TGNP, Catherine Mzurikwao akifuatilia mjadala wakati wa kutengeneza mpango kazi wa kutokomeza ukatili wa kijinsia katika kata ya Lunguya
Mwezeshaji kutoka TGNP, Deogratius Temba akijadili jambo na wazee wa mila ambao ni Wacheza ngoma ya mapacha 'Ukango'
Washiriki wa mdahalo wakitengeneza mpango kazi wa namna ya kutokomeza ukatili wa kijinsia
Washiriki wa mdahalo wakitengeneza mpango kazi wa namna ya kutokomeza ukatili wa kijinsia.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Soma pia:

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments