CHINA YAZINDUA PASIPOTI ZA CORONA KURAHISHA USAFIRI WA KUVUKA MIPAKA


China imezindua programu ya vyeti vya afya kwa wasafiri wa ndani, ikiongoza dunia katika mipango ya kuanzisha kitu kinachoitwa hati za kusafiria za virusi.

Cheti hicho cha kidigitali, ambacho kinaonyesha hali ya chanjo ya mmiliki na matokeo ya kipimo cha virusi, kinatolewa kwa wakazi wote wa China kwa kutumia programu ya mitandao ya kijamii ya WeChat ambayo ilizinduliwa jana Jumatatu.

Cheti hicho kinatolewa "kusaidia kuendeleza kufufua uchumi wa dunia na kurahisisha usafiri wa kuvuka mipaka," wizara ya mambo ya nje ilisema.

Hata hivyo cheti cha kimataifa cha afya kwa sasa kinatolewa tu kwa raia wa China na si lazima.

Cheti hicho, ambacho pia kinapatikana kwa njia ya karatasi, kinafikiriwa kuwa ni "pasipoti ya kwanza duniani ya virusi".

Marekani na Uingereza ni miongoni mwa nchi ambazo kwa sasa zinafikiria kuanzisha cheti kama hicho.

Umoja wa Ulaya pia unafanyia kazi "cheti cha ruhusa" ya chanjo ambacho kitaruhusu wakazi kusafiri ndani ya nchi wanachama na nje.
Programu ya inajumuisha namba maalum ya siri (QR code) ambayo inaruhusu kila nchi kupata taarifa za afya ya msafiri, shirika la habari la serikali, Xinhua liliripoti jana.

"QR codes" ndani ya WeChat na katika programu ya simu janja katika nchi nyingine tayari zinahitajika kuwezesha kutumia usafiri wa ndani na kuingia katika maeneo ya umma.

Programu tumishi hiyo (app) inafuatilia sehemu aliyopo mtumiaji na kutoa namba ya "kijani", ikimaanisha afya nzuri kama mtumiaji hajakaribiana na mtu ambaye amethibitishwa kuwa na maambukizi au hajasafiri kwenda maeneo yenye maambukizi.

Lakini mfumo huo umeibua wasiwasi na woga kuwa unaongeza wigo wa serikali kufuatilia wananchi.

 CHANZO - MWANANCHI


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post