JAMAA AWATENGENEZEA VIATU MAALUMU NG'OMBE WAKE..AANZA KUPIGA HELA KWA WANAOTAKA


Mkulima mmoja Kirinyanga  nchini Kenya Josephat amewatengenezea ng'ombe wake viatu spesheli/maalum ili kulinda kwato zao baada ya kugundua kwamba walikuwa wanachechemea kutokana na miguu yao kuvimba.

Josephat Kariuki kutoka Kutus alisema alitumia magurudumu ya pikipiki na vipande vya nguo kuwatengenezea wanyama hao viatu ili kulinda miguu yao dhidi ya kuvimba.

Akizungumza na stesheni moja ya televisehni nchini, Kariuki amesema alikuwa na kibarua kigumu mara ya kwanza kuwavisha ng'ombe hao viatu.

Amesema japo ng'ombe hao walidinda kuvalia viatu hivyo mara ya kwanza, hatimaye walikubali na kusalia watulivu kila wanapovishwa 

Lakini muda ulipozidi kusonga, ng'ombe hao walianza kuzoea kuvishwa viatu na kuwa watulivu kila mara Kariuki anapowashughulikia.

Kutokana na wazo hilo ndiyo mkulima huyo aliamua kutengeneza viatu vya ng'ombe nyumbani kwake na kuanza kuvuna pesa kwa kuwauzia wafugaji wengine. 

Alisema huwa anaviuza viatu vya ng'ombe kwa KSh400 akiongezea kuwa ana wateja wengi huku viatu hivyo vikithibitisha uwezo wa kulinda kwato za wanyama hao.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post