MWILI WA MAGUFULI KULALA IKULU YA ZANZIBAR LEO, KESHO KUAGWA MWANZA

 
WAZIRI Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya mazishi Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi kuzungumza na Wananchi katika hafla ya kuuaga mwili wa Hayati Dkt.Jon Pombe Magufuli katika uwanja wa Amaan Zanzibar.(Picha na Ikulu)
**
Na Alex Sonna

 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa amesema kuwa Mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dkt. John Magufuli utalala Ikulu Zanzibar leo Machi 23, 2021 na kesho asubuhi utapelekwa jijini Mwanza kwa ajili ya wakazi wa kanda ya ziwa naona kupata nafasi ya kuaga.

Majaliwa ameyasema hayo leo Machi 23,2021 visiwani Zanzibar wakati wa shughuli ya kumuaga Hayati Dkt.John Magufuli iliyofanyika kwenye uwanja wa Amaan Zanzibar 

“”Leo mtapata fursa ya kupita mmoja mmoja mbele ya jeneza na kumuaga, tunaamini kwa idadi hii haiwezi kutuchukua masaa mengi lakini tutakuwa hapa hata kama tutamaliza saa sita usiku, ili mradi kila mmoja anamaliza kiu ya kumuaga Kiongozi wetu””amesema Majaliwa 

Aidha Majaliwa amesema kuwa Kesho asubuhi mwili utaondoka kwenda jijini Mwanza mara baada ya kuagwa mwili  utatembea kwa gari kupita daraja la Busisi na kisha kusimama kwa dakika 10 nyumbani kwa wazazi wa mke wa marehemu.

Chanzo - Fullshangwe blog


UPDATES ZOTE

Pakua / Download App ya Malunde 1 blog Tuwe tunakutumia taarifa zote moja kwa moja kwenye simu yako bure kabisa 

Bofya <<HAPA>> Mara Moja Tu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post