MBUNGE KEMBAKI KUENDESHA HARAMBEE KUNUSURU WANAFUNZI ZAIDI YA 100 KURUNDIKANA DARASA MOJA SHULE YA BUHEMBA

Mbunge wa jimbo la Tarime mjini Michael Kembaki na baadhi ya viongozi wa CCM wakiwa shule ya msingi Buhemba wakati wa Ziara yake ya kukagua miradi ya ujenzi
Mbunge wa jimbo la Tarime mjini Michael Kembaki na baadhi ya viongozi wa CCM wakiwa shule ya msingi Buhemba wakati wa Ziara yake ya kukagua miradi ya ujenzi
Mbunge wa jimbo la Tarime mjini Michael Kembaki na baadhi ya viongozi wa CCM wakiwa shule ya msingi Buhemba wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya ujenzi
**

Na Dinna Maningo, TARIME

Zaidi ya wanafunzi 100 wa darasa la awali (Chekechea) katika shule ya msingi Buhemba kata ya Bomani wilayani Tarime mkoa wa Mara, wanalazimika kurundikana darasa moja lisilo na sakafu wengine kusoma wakiwa wameketi chini kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa.

Hayo yalibainika wakati wa ziara ya Mbunge wa jimbo la Tarime mjini Michael Kembaki wakati akitembelea miradi mbalimbali ya ujenzi ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa na ujenzi wa moja ya barabara za mjini unaotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami.

Mbunge huyo aliongozana na Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya mji Tarime ambaye pia ni Diwani kata ya Nyamisangura Thobias Ghati,Diwani wa kata ya Turwa Chacha Marwa, Katibu wa Chama cha  Mapinduzi wilaya ya Tarime,Mkaruka Kura na katibu Mwenezi wa CCM wilaya hiyo Marema Sollo.

Mkuu wa shule ya msingi Buhemba Kordine Kivuyo alisema kuwa darasa moja wanatakiwa kukaa wanafunzi wa awali 25 hivyo kuna upungufu wa vyumba vinne vya madarasa kwa wanafunzi hao.

"Darasa moja halitoshi kwa kuwa hakuna madarasa wanalazimika kurundikana darasa moja,wanafunzi wa awali wanatakiwa kukaa 25 kwenye darasa moja na baadhi ya wanafunzi wanakaa chini darasa halina sakafu wanabanana inakuwa kero kwao,mwalimu anapata shida kufundisha ikizingatiwa ni watoto wadogo wanahitaji mazingira rafiki inakuwa rahisi katika ufundishaji", alisema Kivuyo.

Mkuu huyo wa shule alisema kuwa shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 1,400 kati ya hao wavulana ni 669 na wasichana 731,madarasa yanayohitajika ni 32 yaliyopo 14 pungufu 18,madawati yanahitajika 482 yaliyopo 291 pungufu 191,matundu ya vyoo yanahitajika 64 yaliyopo 10 pungufu 54.

"Walimu wanaohitajika ni  32 waliopo 24 pungufu walimu nane,nyumba za walimu zilizopo ni mbili,tunahitaji printa na mashine ya photocopy, madarasa matatu hayana sakafu, tumejitahidi kutatua baadhi ya changamoto kama ukarabati wa madawati,tunaumeme ambao umetusaidia kupunguza gharama za uchapaji mitihani,tuna maji ya bomba na shamba la shule kwa ajili ya kilimo kinachowawezesha wanafunzi kupata maarifa", alisema.

Mkuu huyo alisema kuwa ufaulu umekuwa ukiongezeka kila mwaka, 2018 wanafunzi waliohitimu darasa la saba na kufanya mtihani walikuwa 155 waliofaulu walikuwa 135, mwaka 2019 waliofanya mtihani walikuwa 137 waliofaulu 119 , 2020 waliofanya mtihani walikuwa 153 waliofaulu 143 na kwa upande wa darasa la nne ufaulu ukipanda kwa asilimia 96.

Alisema kuwa katika ujenzi wa madarasa matatu wananchi wamechangia nguvu kazi na fedha kiasi cha milioni 1.6 ambazo zimetumika kwenye ujenzi hatua ya msingi.

Kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa, Mbunge Kembaki aliahidi kufanya harambee ambayo ataalika wadau mbalimbali kuchangia fedha kujenga madarasa ili kuondokana na changamoto ya uhaba wa madarasa huku akipongeza uongozi wa shule kwa kazi wanayofanya kuhakikisha taaluma inakuwa vizuri.

"Bado tuna changamoto za kitaaluma kama upungufu wa walimu, vyumba vya madarasa, madawati na mahitaji mengine kwakuwa mmenipa kazi ya kushawishi wananchi kuchangia maendeleo ya shule nitafanya harambee tupate fedha na siku ya harambee nitawaletea printa nimefurahishwa mmejenga msingi wa vyumba vitatu vya madarasa tena kwa gharama ndogo kuna maeneo mengine misingi imejengwa kwa gharama kubwa ya fedha",alisema Kembaki.

Mbunge huyo aliwataka walimu kuhakikisha wanawajibika vilivyo kuhudhuria vipindi vyote darasani ili kuinua taaluma nakuahidi kutoa ushirikiano kuhakikisha shughuli za maendeleo zinafanyika ili kupunguza changamoto za shule.

Mjumbe wa kamati ya shule hiyo Gweso Nyakisagane alisisitiza ujenzi wa vyumba vya madarasa hasa kwa wanafunzi wa chekechea ambao umesababisha wanafunzi kusoma katika Mazingira magumu na akaipongeza serikali ya awamu ya tano katika jitihada zake kuhakikisha maendeleo yanakuwa hara

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post