KAKA WAWILI WAUANA BAADA YA WAKE ZAO KUCHAPANA MAKONDE

Wananchi wakiwa eneo la tukio
**
Wenyeji wa Kaniga Makome eneo bunge la Muhoroni, kaunti ya Kisumu nchini Kenya wameachwa midomo wazi kufuatia kisa kilichoplekea kaka wawili kupoteza uhai wao. 

Wakazi waliomboleza kaka hao Joseph Othoro na Kennedy Otieno ila ndani yao maswali mengi yalibaki bila majibu kuhusu tukio hilo la kuogofya.

Otoro mwenye umri wa miaka 37 aliaga dunia usiku wa Jumatatu, Machi 1,2021 huku mdogo wake Otieno (36) akifuata mapema asubuhi siku iliyofuata. 

Kulingana na ripoti ya polisi , ndugu hao wawili walishambuliana kwa saa kadhaa usiku wa Machi 1,2021 na walipata majeraha ambayo yalisababisha vifo vyao.

 Mzozo baina yao uliibuka wakati wake zao walitandikana Jumapili, Februari 28,2021 hatua ambayo ilizidisha hasira kati ya Othoro na Otieno usiku huo.

Kaka hao walishambuliana bila huruma na kutokana na majeraha waliyokuwa nayo walikimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu.

 Otieno aliaga dunia wakati akikimbizwa hospitalini usiku naye Othoro alithibitishwa kufuata baadaye asubuhi ya Jumanne, Machi 2,2021.

Chanzo - Tuko News


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post