ASKOFU GWAJIMA : RAIS SAMIA NI KONKI FIRE...YUPO JUU MAWINGUNI

Mbunge wa Jimbo la Kawe Mhe. Askofu Josephat Gwajima

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mbunge wa Jimbo la Kawe Mhe. Askofu Josephat Gwajima amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia kumpendekeza Waziri wa Fedha na MipangoDkt. Philip Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Jina la Dkt. Mpango limesomwa bungeni jijini Dodoma leo Jumanne Machi 30, 2021 na Spika Job Ndugai aliyeletewa bahasha yenye jina hilo na mpambe wa kiongozi mkuu huyo wa nchi.

Akizungumza bungeni, Mbunge Gwajima amesema Dkt. Philip Mpango ni Mpango kweli kweli.

"Tumezoea kuwanukuu wanafalsafa mbalimbali duniani, lakini leo nataka nimnukuu Mtanzania mmoja anayeitwa Pierre Liquid ...Niseme Mama Samia ni Konki Fire, Mama Samia yupo juu Mawinguni na yupo juu sana ndiyo maana kwa jicho lake amefanikiwa kumuona na kumteua Dkt. Philip Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Jicho lililomuona Dkt. Mpango ni kubwa kuliko la aliyependezewa, Dkt Philip Mpango ni Mpango kweli kweli",amesema Gwajima.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post