NAIBU WAZIRI VIWANDA NA BIASHARA AKUTANA NA WADAU WA SEKTA YA NGUO NA MAVAZI JIJINI DODOMA

 

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe,akizungumza na wadau wa Sekta ya Nguo na Mavazi alipokutana nao ili kisikiliza changamoto wanazokutana nazo katika uendelezaji wa Viwanda na biashara ya nguo na mavazi nchini jijini Dodoma

Katibu wa Jumuiya ya Wafanyabishara Tanzania (JWT) Bw. Abdala Mwinyi akiwasilisha changamoto zinazowakabili wafanyabiashara wa nguo na mavazi hususan vitenge kwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe(MB) katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma

Wadau wa sekta ya nguo na mavazi wakiwa katika kikao cha pamoja na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe, chenye lengo la kisikiliza na kutatua changamoto wanazokutana nazo katika uendelezaji wa Viwanda na biashara ya nguo na mavazi nchinikilichofanyika jijini Dodoma

Katibu Mtendaji wa Chama cha Wazalishaji Nguo na Mavazi Tanzania TEGAMAT akiwasilisha changamoto zinazowakabili wanachama wake kwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe(MB) alipokutana na wadau wa Sekta ya Nguo na Mavazi ili kisikiliza changamoto wanazokutana nazo katika uendelezaji wa Viwanda na biashara ya nguo na mavazi nchini kilichofanyika jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe, akifafanua jambo kwa wazalishaji na waagizaji wa nguo na mavazi hususani vitenge na kanga katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma

Baadhi ya Waagizaji wa nguo na mavazi hususan vitenge kutoka nje ya nchi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe(MB) (hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma


Na.Alex Sonna,Dodoma

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe amekutana na kufanya mazungumzo na wadau wa sekta ya nguo na mavazi ili kusikiliza changamoto wanazokutana nazo na mapendekezo yao katika kuboresha na kukuza sekta hiyo.

Akizungumza na wadau hao katika kikao kilichofanyika leo tarehe 9 Februari 2021 jijini Dodoma Mhe Kigahe aliwaagiza kuwasilisha changamoto walizonazo na rasimu za mipango mikakati ya kuboresha na kuendeleza Viwanda na Biashara katika sekta hiyo ili kukuza uchumi wa nchi.

Aidha katika kikao hicho kilichojumuisha wadau ambao ni watengenezaji na waagizaji wa nguo na mavazi kutoka nje ya nchi, wadau hao waliwasilisha changamoto na mapendekezo yao kwa Mhe. Naibu Waziri wakiwa na lengo la kuboresha na kukuza sekta hiyo.

Aidha, Mhe.Kigahe amesema kuwa Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali katika kuendeleza sekta ya nguo na mavazi nchini ikiwemo kukuza soko la ndani la bidhaa.

Aidha amesema kuwa amekuwa wakianda na kutekeleza Mkakati wa kuendeleza Sekta ya pamba nguo hadi mavazi ( Cotton to Clothing Strategy C2C 2016 - 2020 ) na kuuhuisha ambapo utekelezaji wake utaanza mwaka 2021 - 2032.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post