MBUNGE MANYANYA ATAJA KILICHOSABABISHA CCM KUSHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI MKUU 2020 | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, February 11, 2021

MBUNGE MANYANYA ATAJA KILICHOSABABISHA CCM KUSHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI MKUU 2020

  TANGA RAHA BLOG       Thursday, February 11, 2021

 


Na Alex Sonna, Dodoma

MBUNGE wa Nyasa(CCM), Mhandisi Stella Manyanya, amesema sababu za Chama cha Mapinduzi(CCM), kushinda kwa kishindo kwenye uchaguzi mkuu 2020 ni kutokana na mambo yaliyofanywa na serikali chini ya Rais Dk.John Magufuli.

Akichangia Mpango wa tatu wa Maendeleo wa Miaka mitano bungeni leo, Manyanya amesema wananchi wameelewa namna ambavyo CCM imetekeleza yale yaliyoahidiwa na masikio yao kwasasa wasikiliza mpango huo utawasaidiaje.

“Mpango huu utakuwa na maana zaidi pale tutakapohakikisha unakuwa na manufaa kwa watanzania,”amesema.

Aidha, ameishauri serikali kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa bwawa la uzalishaji umeme la Mwalimu Nyerere na ujenzi wa reli ya kisasa katika Mpango huo kwa kuwa miradi hiyo ni mkombozi kwa watanzania.

“Inahitaji mtu ambaye hakuwepo kwenye mgao wa umeme ashangae Bwawa la Nyerere, ni mtu atakayeshindwa kujua tunapoteza mapato kutokana na usafirishaji mizigo kutoa bandarini kupeleka nchi jirani, wana CCM tuna wajibu wa kuelimisha wananchi ili kujua umuhimu wa miradi hii mikubwa,tuendelee kuisemea hadi itakapokamilika,”amesema.

Ameomba serikali kukamilisha miradi hiyo ili isaide upatikanaji wa fedha nyingi za kuhudumia maeneo mbalimbali katika nchi.

“Tuwe na fedha kidogo au zaidi lazima miradi hii ya kimkakati ikamilike, pia tuimalishe ulinzi wa mipaka yetu,”amesema.

Aidha, amesema maendeleo yanakwenda kwa kasi Nyasa na Mbinga kutokana ujenzi wa barabara uliofanywa.

“Niombe yale yaliyoainishwa kwenye Ilani ya uchaguzi ya CCM barabara ya Chiwindi-Mbambay hadi Litui-Amani makoro na daraja la mitomoni kipande kile kinadai katika mpango huu mambo yatekelezwe kama yalivyoahidiwa,”amesema.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post