MADIWANI WAANZA MIKAKATI KUIPANDISHA HADHI MANISPAA YA SHINYANGA KUWA JIJI.... DC MBONEKO AAGIZA KASI UKUSANYAJI MAPATO

 

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Bajeti la Madiwani Manispaa ya Shinyanga.

Na Marco Maduhu, Shinyanga
Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wameanza kupanga mipango ya kimkakati ya kuipandisha hadhi manispaa hiyo kuwa Jiji.

Meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila, amewasilisha leo jambo la dharura kwenye kikao cha Bajeti cha Baraza la Madiwani, kuwa kuna haja ya Manispaa hiyo kuipandisha hadhi ya Jiji ikiwa uwezo wanao.

Amesema Halmashauri ya mji wa Kahama kupandishwa hadhi na Mheshimiwa Rais John Magufuli kuwa Manispaa ni changamoto kwao, ambapo na wao lazima wapambane na kupanda hadhi kuwa Jijij la Shinyanga, na siyo Manispaa tena.

“Madiwani hakuna kitu ambacho kitatu kwamisha kutoka kwenye Manispaa na kuwa Jiji sababu watalaamu wa uchumi tunao, uwezo wa kuibua vyanzo vipya ya mapato tunao, pamoja na maeneo ya uwekezaji tunayo, likiwamo na eneo la Tanganyika pekazi ambalo tunataka tukabidhiziwe rasmi ,”amesema Nkulila.

Nao Madiwani wa Halmashauri hiyo akiwamo Mariam Nyangaka, wamepongeza mipango hiyo ya kuipandisha hadhi Manispaa ya Shinyanga kuwa Jiji, huku wakiahidi kushirikiana kikamilifu kwenye mipango na kutimiza malengo ambayo wamejiwekea.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, amepongea mipango hiyo ya kuipandisha manispaa ya Shinyanga kuwa hadhi ya Jiji, na kusisitiza ili kufikia malengo hayo lazima kasi iongezwe ya ukusanyaji mapato, pamoja na kuibua vyanzo vipya, ili fedha ipatikane ya kutekeleza malengo yao ya kufikia hadhi ya jiji ikiwamo na miradi ya maendeleo.

“Suala la ukusanyaji mapato ni la muhimu sana, hakuna Halmashauri bila mapato, tuongeze kasi ya ukusanyaji mapato pamoja na kuibua vyanzo vipya, ili tupate mapato mengi na kutimiza malengo ya kufikia hadhi ya Jiji,”amesema Mboneko.

Katika hatua nyingine amesisitiza suala la upimaji wa viwanja, pamoja na kuwabana wadaiwa sugu, ili yapatikane mapato, fedha ambazo zitatekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi.

Aidha baraza hilo la Halmashauri manispaa ya Shinyanga, limejadili ajenga mbalimbali kwa ajili wa mstakabali wa maendeleo ya wananchi wa manispaa hiyo, ikiwamo miundombinu ya barabara, maji, elimu, umeme, afya, uchumi, mikopo ya wanawake, vijana, na walemavu, ambapo kesho watajadili na kupitisha mapendekezo ya mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha (2021-2022).

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye kikao cha Bajeti cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiendelea kusisitiza jambo kwenye kikao cha Bajeti cha Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga, likiwemo suala la usafi wa mazingira, ujenzi vyumba madarasa. pamoja na Maofisa kilimo kutoa elimu kwa wakulima kulima kilimo chenye tija.
Meya wa Mansipaa ya Shinyanga David Nkulila, akizungumza kwenye kikao cha Bajeti cha Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga.
Meya wa Mansipaa ya Shinyanga David Nkulila, akisisitiza jambo kwenye kikao cha Bajeti cha Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi, akizungumza kwenye kikao cha Bajeti cha Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga.
Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha Baraza la Bajeti.
Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha Baraza la Bajeti.
Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha Baraza la Bajeti.
Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha Baraza la Bajeti.
Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha Baraza la Bajeti.
Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha Baraza la Bajeti.
Diwani wa Kitangili Mariam Nyangaka, akichangia ajenda kwenye Baraza hilo.
Diwani wa Ibinzamata Ezekiel Sabo, akichangia ajenda kwenye Baraza hilo.
Diwani wa Chibe John Kisandu,akichangia ajenda kwenye Baraza hilo.
Wakuu wa idara wa manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye Baraza hilo.
Kikao cha Baraza kikiendelea.
Kikao cha Baraza kikiendelea.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post