BABU WA MIAKA 72 AJIUA KWA HASIRA KUSHTAKIWA POLISI NA MKEWE

Na Fina Lyimo - Mwananchi
Mkazi wa Kijiji cha Lyamungo Sinde, Zephania Lyimo (72) anadaiwa kujinyonga kwa kutumia kamba ya manila kwa madai ya kukasirishwa na mkewe kumshtaki polisi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Ronald Makona alidai kuwa Lyimo alikutwa amejinyonga kwa kamba sebuleni kwake Januari 31 mwaka huu, lakini ndugu wanadai kiini ni tukio hilo la mkewe, Mary.

Kamanda Makona alisema juzi kuwa mzee huyo alikutwa ananing’inia na hakuacha ujumbe wowote unaoelezea sababu za kuchukua uamuzi huo.

“Alikuwa amefunga kamba hiyo kwenye kenchi ya paa la sebuleni, taarifa ya chanzo cha kuamua kufanya hivyo hazikujulikana mara moja,” alisema kamanda huyo wa polisi.

Hata hivyo, mke wa marehemu, Mary Lyimo alisema alifikia uamuzi wa kumpeleka mumewe katika dawati la jinsia Kituo cha Polisi Hai baada ya kuishi miaka mingi akiteseka kwa vipigo.

Alidai kuwa alifika polisi na kujieleza kisha mumewe aliitwa Januari 27 na kusomewa mashtaka ambayo ni kumpiga mkewe na kumfungia nje mara kwa mara.

“Kwa kuwa mume wangu ni mkorofi alikuwa anakataa kuwa hanifanyii ukatili huo, yule askari alisema akachapwe viboko, ili atulie na ndipo walipomchukua na kwenda kumweka rumande,”alidai mwanamke huyo.

“Baada ya saa saba kupita, mkwe wangu ambaye ni mume wa mwanangu anayeishi Arusha alipigiwa simu na kuja kumwekea dhamana, tukasuluhishwa, tukaambiwa Ijumaa ya Januari 29 turudi kueleza kama tumeelewana,” alidai Mary.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post