WALIOIGIZA MCHEZO WA MKE NA MME UTOTONI WAOANA RASMI


Urafiki ambao ulianza 1995 umegeuka ndoa ambapo Mnamo Jumanne, Februari 16,2021 picha ziliibuka kwenye mtandao wa Twitter za wanandoa ambao wamefanya harusi hivi majuzi.

Katika picha hizo mtandaoni kwenye kitandazi cha Twtter cha @CWekuNii, picha moja inawaonyesha wapenzi hao wakiwa watoto na kuvalia mavazi ya harusi ambayo wanadaiwa kuvaa wakiigiza mchezo katika shule ya msingi.

Ujumbe kwenye posti hiyo unasema: "Mpendwa Ama.. ninataka kutumia fursa hii kukushukuru. Tulikuwa katika shule ya msingi mwaka 1995 wakati tuliigiza mchezo pamoja uliokuwa umeandaliwa na shule.Tangu siku hiyo tumekuwa marafiki wa kufa kuzikana hadi sasa. Tumefika hapa sasa. Mungu na abariki ndoa yetu."

Wanandoa hao wameonyesha matumaini kwamba kuna mapenzi ya kweli baada ya picha zao za harusi kusambaa mitandaoni.

Katika picha hizo mtandaoni kwenye kitandazi cha Twitter cha @CWekuNii, picha ya utotoni ya wawili hao inawaonyesha wakiwa wamevalia mavazi ya harusi.

Wengi walifurahishwa na safari yao ya mapenzi na kuwaombea furaha katika ndoa yao

Wanamtandao wengi walifurahishwa na safari yao ya mapenzi na kuwaombea furaha katika ndoa yao.

Chanzo- Tuko News

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post