MWILI WA MAALIM SEIF WAAGWA DAR


Mwili wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, umeagwa mapema leo asubuhi katika msikiti wa Maamur Upanga jijini Dar es Salaam kabla ya kupelekwa Zanzibar kwa ajili ya mazishi.

Dua maalum ya kumuombea Maalim Seif imeongozwa na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuberi, ambapo amesema kuwa msiba huu umeathiri watu wengi kwa sababu Maalim Seif alikuwepo kwa ajili ya Watanzania wote

Akizungumza wakati wa Dua hiyo Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum, amesema kuwa watu wanajua juhudi ambazo Maalim Seif, alizifanya na si kwa Wazanzibar pekee bali kwa Watanzania wote na kwamba ataendelea kukumbukwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar.

Wakazi wa jiji la Dar es salaam wamejitokeza kwa wingi kumswalia Makamu wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Seif Sharif Hamad.

Viongozi mbalimbali pia wameshiriki ibada hiyo akiwemo Rais mstaafu Jakaya Mrisho kikwete na Kiongozi wa ACT Zitto Kabwe.

Baadhi ya waliohudhuria ibada hii wamesema kuwa wamesikitishwa sana na msiba huu, baadhi yao wamewahi kusaidiwa kwa namna moja ama nyingine na Maalim Seif.

Maalim Seif atazikwa leo Februari 18, 2021, huko Mtambwe, Pemba visiwani Zanzibar.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post