Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Benki ya
CRDB Tawi la Shinyanga imezindua rasmi Huduma za fedha kupitia Simu ya mkononi 'Sim
Banking' iliyoboreshwa kupewa jina la Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ itakayowawezesha wateja kufanya huduma zote za
kibenki kupitia simu zao popote walipo.
Uzinduzi huo
umefanyika leo Alhamisi Februari 25,2021 katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
ukiongozwa na Meneja wa Benki hiyo, Luther Mneney na kuhudhuriwa na wateja na
wafanyakazi wa benki hiyo.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo, Mneney amesema Huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo
Umeboreshwa’ itafanyika katika matawi yote na itawawezesha wateja kupata huduma
nyingi zaidi za kibenki kupitia simu ya mkononi na kwa urahisi zaidi ili kufurahia benki ya CRDB.
“Ukiwa ni simu basi una huduma zote za kibenki kidigitali zaidi. Benki ni
SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ inachukua nafasi ya huduma yetu ya mwanzo ya
Simbanking lakini hii ni babu kubwa, tumeiboresha sana ili kuwafanya wateja
wafurahie huduma zetu”,amesema Mneney.
“Wanachotakiwa
kufanya wateja wetu kupiga *150*03# au kupakua CRDB SimBanking Playstore au
Appstore na kupata huduma za kibenki zilizoboreshwa zaidi”,amesema Mneney.
Akielezea
kuhusu Benki ni SimBanking ‘ Mzigo Umeboreshwa’, Afisa wa Benki ya CRDB, Lewis
Temu amesema kupitia huduma hiyo yenye mpangilio mzuri, wateja wataweza pia
kupata huduma za bima kiganjani ambapo TIRA imeunganishwa.
“Mteja
atafungua akaunti kwa kutumia namba ya NIDA, kuhamisha fedha kirahisi,kutoa
fedha kwenye ATM,matawi na mawakala,uwezo wa kurekodi miamala yote,kupata
taarifa,kupata token ya umem papo hapo,kufunga na kufungua kadi,kuomba kadi,kulipia
luku. DSTV na huduma zingine kabambe ikiwa ni pamoja na kutoa fedha hadi
shilingi milioni 8”,amesema Temu.
Meneja wa
Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui amesema wameamua kuboresha huduma za
kibenki mara kwa mara kutokana na
mahitaji makubwa ya wateja kiuchumi ndiyo wameamua kuja na mzigo mpya
ulioboreshwa na kuwaomba wateja waliohudhuria uzinduzi huo kuwa mabalozi
wazuri.
Naye Meneja Biashara wa CRDB Kanda ya Magharibi,Jumanne Wagana alimtangaza Mkurugenzi wa
Malunde 1 blog, Kadama Malunde kuwa Balozi wa Benki ni SimBanking ‘ Mzigo
Umeboreshwa’ Kanda ya Magharibi akisema Malunde 1 blog ni mtandao wa kijamii unaofanya vizuri
nchini Tanzania.
Akizungumza
kwa niaba ya wateja waliohudhuria uzinduzi huo, Barikiel Somboi ameipongeza
Benki ya CRDB kwa kuendelea kufanya ubunifu mara kwa mara ili kukidhi mahitaji
ya wateja.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney akizungumza leo Alhamis Februari 25,2021 wakati wa uzinduzi wa huduma ya fedha kupitia simu 'Sim Banking' iliyoboreshwa kupewa jina la Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ itakayowawezesha wateja kufanya huduma zote za kibenki kupitia simu. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney akizungumza leo Alhamis Februari 25,2021 wakati wa uzinduzi wa huduma ya fedha kupitia simu 'Sim Banking' iliyoboreshwa kupewa jina la Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ itakayowawezesha wateja kufanya huduma zote za kibenki kupitia simu.
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney akizungumza leo Alhamis Februari 25,2021 wakati wa uzinduzi wa huduma ya fedha kupitia simu 'Sim Banking' iliyoboreshwa kupewa jina la Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ itakayowawezesha wateja kufanya huduma zote za kibenki kupitia simu.
Afisa wa Benki ya CRDB, Lewis Temu akielezea kuhusu Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’.
Afisa wa Benki ya CRDB, Lewis Temu akielezea kuhusu Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’.
Keki na vinywaji mbalimbali wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ' Mzigo Umeboreshwa' katika benki ya CRDB Tawi la Shinyanga.
Meneja Biashara Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Mwanahamis Iddi akifungua Keki maalumu kwa ajili ya uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Keki maalumu kwa ajili ya uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Meneja Biashara Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Mwanahamis Iddi akizungumza wakati wa zoezi la kukata keki maalumu kwa ajili ya uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Mteja wa Benki ya CRDB Joab Kaijage akikata Keki maalumu kwa ajili ya uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Mteja wa Benki ya CRDB Joab Kaijage akikata Keki maalumu kwa ajili ya uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Mteja wa Benki ya CRDB Joab Kaijage akikata Keki maalumu kwa ajili ya uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney (kulia) akimlisha keki mteja wa Benki ya CRDB Joab Kaijage wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Mteja wa Benki ya CRDB Joab Kaijage (kushoto) akimlisha keki Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Mteja wa Benki ya CRDB Joab Kaijage (kulia) akimlisha keki Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney (kulia) akimlisha keki mteja wa Benki ya CRDB wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney (kulia) akimlisha keki mteja wa Benki ya CRDB wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney (kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney (kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney (kulia) akijiandaa kugawa keki kwa wateja na wafanyakazi wa benki ya CRDB wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Mteja wa Benki ya CRDB, Barikiel Somboi akiipongeza benki hiyo kwa kuendelea kuboresha huduma za kibenki akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiwa ndani ya benki ya CRDB wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana (kushoto) akimkabidhi Note Book ya Benki ya CRDB, Mkurugenzi wa Mtandao wa Habari wa Malunde 1 blog, Kadama Malunde baada ya kumtangaza kuwa Balozi wa 'Benki ni SimBanking' Kanda ya Magharibi wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui (kushoto), Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana na Meneja Biashara Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Mwanahamisi Iddi wakigonga Cheers wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Afisa Biashara Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Mwanahamisi Iddi akimhudumia vitafunwa mteja wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui akigonga cheers na wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui akigonga cheers na wafanyakazi wa benki ya CRDB wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiwa ndani ya benki wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga
Picha ya pamoja wateja na wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking ‘Mzigo Umeboreshwa’ katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com