BENKI YA CRDB YAZINDUA HUDUMA YA ‘BENKI NI SIMBANKING’ JIJINI MWANZA


Katika kuendelea kuboresha huduma zake, benki ya CRDB Kanda ya Ziwa imezindua huduma ya Benki ni SimBanking 'Mzigo Umeboreshwa inayowawezesha wateja wake kupata huduma za kifedha popote walipo kupitia simu zao za mkononi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika Februari 25, 2021 katika tawi la Rock City Mall jijini Mwanza, Meneja wa CRDB Kanda ya Ziwa Lusingi Sitta alisema huduma hiyo inawarahisishia wateja kutoa pesa, kuhamisha pesa, kufanya malipo ya Serikali huku pia usalama wa akaunti ya mteja ukiimarishwa zaidi.

Aidha Sitta aliongeza kuwa huduma nyingine zilizoboreshwa ni urahisi wa kupata mikopo mbalimbali, taarifa za mihamala ya fedha, kutoa pesa kwa mawakala na mashine za ATM bila kuwa na kadi ya benki na hivyo kuwahimiza wananchi kuchangamkia huduma hiyo kwani sasa hakuna sababu ya kwenda ndani ya benki kufuata huduma za kifedha kwa kuwa zote zinapatikana kiganjani.

Naye Meneja Biashara Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa, Japhary Hassanaly alisema wateja wa benki hiyo wanaweza kufurahia huduma ya SimBaking wakiwa na aina yoyote ya simu za kiganjani.
"Ukiwa hata na simu ya tochi unaweza kupata huduma kwa kubonyeza *150*03# lakini kwa wale wenye simu janja wanaweza kupakua 'SimBanking App' na kwa uharaka wakapata huduma" alisema Hassanaly.

Mmoja wa wateja wa CRDB, Nadhifa Said ambaye pia ni Rais wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo cha IFM tawi la Mwanza alisema huduma hiyo itawarahisishia mahitaji yao popote wanapokuwa ikiwepo mkopo wa awali wakati wanasubiri 'boom' na hivyo kuwahimiza wanafunzi na wateja wengine wa benki hiyo kupakua 'SimBanking App' kwani Mzigo Umeboreshwa.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Meneja wa CRDB Kanda ya Ziwa Lusingi Sitta (wa pili kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking 'Mzigo Umeboreshwa" uliofanyika katika tawi la Rock City jijini Mwanza. Kitaifa uzinduzi huo ulifanyika Februari 24, 2021 jijini Dar es salaam.
Meneja Biashara Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa Japhary Hassanaly (katikati) akifafanua maboresho yaliyofanyika kwenye App ya SimBanking inayopatikana kwa watumiaji wote wa simu janja.
Meneja wa CRDB Kanda ya Ziwa Lusingi Sitta (kushoto) akizungumza jambo kabla ya kukata utepe kuashiria uzinduzi wa huduma ya Benki ni SimBanking 'Mzigo Umeboreshwa' katika tawi la Rock City jijini Mwanza.
Viongozi wa CRDB wakiwa kwenye picha ya pamoja na wateja wa benki hiyo.
Meneja wa CRDB Kanda ya Ziwa Lusingi Sitta (kushoto) akiteta jambo na mateja wa benki hiyo, Nadhifa Said (kulia) ambaye pia ni Rais wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo cha IFM tawi la Mwanza.
Benki ni SimBanking 'Mzigo Umeboreshwa'
Tazama BMG TV hapa chini

Soma Pia :BENKI YA CRDB SHINYANGA YAZINDUA RASMI HUDUMA YA 'BENKI NI SIMBANKING' MZIGO UMEBORESHWA...MALUNDE ALAMBA UBALOZI


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post