WAZIRI NDAKI AZINDUA MWONGOZO WA UTOAJI WA CHANJO ZA MIFUGO NCHINI,ASEMA UTALINDA AFYA YA MNYAMA

 

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa utaoaji chanjo dhidi ya magonjwa ya mifungo kwa mfumo wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi iliyofanyika jijini Dodoma Januari 22,2021.

Baadhi ya wadau wa Sekta ya Mifugo wakifatilia hotuba ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki wakati akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa utaoaji chanjo dhidi ya magonjwa ya mifungo kwa mfumo wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi iliyofanyika jijini Dodoma Januari 22,2021.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Pauline Gekul,akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa utaoaji chanjo dhidi ya magonjwa ya mifungo kwa mfumo wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi iliyofanyika jijini Dodoma Januari 22,2021.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo prof. Elisante Ole Gabriel,akisisitiza jambo kwa wadau wa sekta ya mifugo (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Mwongozo wa utaoaji chanjo dhidi ya magonjwa ya mifungo kwa mfumo wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi iliyofanyika jijini Dodoma Januari 22,2021.

Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mwanahamisi Munkunda,akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwenye uzinduzi wa Mwongozo wa utaoaji chanjo dhidi ya magonjwa ya mifungo kwa mfumo wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi iliyofanyika jijini Dodoma Januari 22,2021.

Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Mhe Jabir Shekimweri ,akitoa maoni kwa niaba ya wakuu wa wilaya zote za Dodoma wakati wa uzinduzi wa Mwongozo wa utaoaji chanjo dhidi ya magonjwa ya mifungo kwa mfumo wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi iliyofanyika jijini Dodoma Januari 22,2021.

Mtaalamu wa kufuatilia Magonjwa ya Mifugo FAO Dkt.Niwael Mtui akiwaelezea wadau wa sekta ya mifugo wakati wa uzinduzi wa Mwongozo wa utaoaji chanjo dhidi ya magonjwa ya mifungo kwa mfumo wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi iliyofanyika jijini Dodoma Januari 22,2021.

Muwakilisha wa wataalamu wa mifugo Wastaafu Tanzania (UWAMIWATA) akichagia wakati wa uzinduzi wa Mwongozo wa utaoaji chanjo dhidi ya magonjwa ya mifungo kwa mfumo wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi iliyofanyika jijini Dodoma Januari 22,2021.

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Dkt.Omary Nkullo akizungumza kwenye uzinduzi wa Mwongozo wa utaoaji chanjo dhidi ya magonjwa ya mifungo kwa mfumo wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi iliyofanyika jijini Dodoma Januari 22,2021.

Baadhi ya wadau wa Sekta ya Mifugo wakifatilia Uzinduzi wa Mwongozo wa utaoaji chanjo dhidi ya magonjwa ya mifungo kwa mfumo wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi iliyofanyika jijini Dodoma Januari 22,2021.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mwongozo wa utaoaji chanjo dhidi ya magonjwa ya mifungo kwa mfumo wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi iliyofanyika jijini Dodoma Januari 22,2021.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki akimkabidhi Naibu Waziri wa wizara hiyo Mhe. Pauline Gekul mwongozo wa utoaji wa chanjo dhidi ya magonjwa ya mifugo nchini kati ya sekta binafsi na umma katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dodoma Januari 22,2021.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe. Mwanahamisi Mukunda, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge, mwongozo wa utoaji wa chanjo dhidi ya magonjwa ya mifugo nchini kati ya sekta binafsi na umma katika hafla iliyofanyika jijini Dodoma Januari 2.2021.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Mashimba Ndaki akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Mhe Jabir Shekimweri,mwongozo wa utoaji wa chanjo dhidi ya magonjwa ya mifugo nchini kati ya sekta binafsi na umma katika hafla iliyofanyika jijini Dodoma Januari 22,2021.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Mashimba Ndaki akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Dk.Suleiman Serera,mwongozo wa utoaji wa chanjo dhidi ya magonjwa ya mifugo nchini kati ya sekta binafsi na umma katika hafla iliyofanyika jijini Dodoma Januari 22,2021.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki akimkabidhi Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji nchini Bw. Jeremiah Wambura mwongozo wa utoaji wa chanjo dhidi ya magonjwa ya mifugo nchini kati ya sekta binafsi na umma katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dodoma Januari 22,2021.

Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji nchini Bw. Jeremiah Wambura akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Mashimba Ndaki mara baada ya kuzindua mwongozo wa utoaji wa chanjo dhidi ya magonjwa ya mifugo nchini kati ya sekta binafsi na umma katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dodoma Januari 22,2021.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua mwongozo wa utoaji wa chanjo dhidi ya magonjwa ya mifugo nchini kati ya sekta binafsi na umma katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dodoma Januari 22,2021.

....................................................................................................

Na.Alex Sonna,Dodoma

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Mashimba Ndaki amezindua mwongozo wa utoaji wa chanjo dhidi ya magonjwa ya mifugo nchini, wenye lengo la kuhakikisha sekta binafsi na umma zinajua haki na wajibu katika zoezi zima la utoaji wa chanjo na kuhakikisha afya ya mnyama inabaki salama.

Mara baada ya kuzindua mwongozo huo jijini Dodoma Januari 22,2021 Mhe.Ndaki aameagiza kusimamishwa kwa muda, utoaji wa chanjo unaofanywa na halmashauri nchini kupitia kampuni walizoingia nazo mikataba, baada ya kubaini chanjo kutolewa kiholela kwa mifugo bila kuwepo utaratibu sahihi na kusababisha madhara kwa mifugo na hasara kwa mfugaji.

Aidha Mhe.Ndaki amesema kuwa katika kuhakikisha mwongozo wa utoaji wa chanjo dhidi ya magonjwa ya mifugo nchini, unakuwa na tija kwa taifa hivyo nataka haki na wajibu kwa kila wadau wa mifugo.

“Hapa tunaangalia afya ya mifugo, afya ya mifugo ilikuwa hatarini ni kweli utaratibu wanafanya halmashauri lakini hauko wazi sana, ndiyo maana tukasema sasa ni muhimu kuwa na mwongozo huu kutuelekeza nini cha kufanya, chanjo ikifanywa vizuri kwa usahihi bila makosa tuliyokuwa tunayaona tunaweza kuwa na ng’ombe wenye afya bora na njema.” Amesema Mhe.Ndaki

Aidha, amesema kuwa mwongozo huo umeshirikisha wadau zaidi ya thelathini wakati wa kuundaa, Wizara ya Mifugo na Uvuvi ipo tayari kupokea maoni ya wadau sehemu ambazo mwongozo utaonekana kuwa na mapungufu ili kuurekebisha na kuufanya uwe bora zaidi, lengo likiwa ni kuhakikisha afya ya mifugo nchini inalindwa na mfugaji kutopata hasara ya mifugo yake kufa au kupata madhara mengine yoyote baada ya kuchanjwa.

Hata hivyo Mhe Ndaki amesema kuwa wizara itahakikisha inaandaa mazingira mazuri ya kuwa pamoja na sekta binafsi ili kufanya kazi pamoja ambayo itakuwa na tija kwa taifa na wafugaji kwa ujumla.

“Sekta binafsi nipende kuwahakikishieni kuwa sisi tutafanya kazi na sekta binafsi vizuri kabisa tusiwe na mashaka ni vile tuliona kasoro, lakini niwaombeni sekta binafsi hasa wale mlio vizuri katika jambo hili la chanjo msiwe na wasiwasi hata mkiingia mikataba na halmashauri ili mradi muwe na sifa na vigezo ndiyo maana ya sisi tukatoa mwongozo ili tufanye kazi pamoja.” Amefafanua Mhe.Ndaki

Hata hivyo Waziri Ndaki amewataka viongozi wenzake wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, mamlaka za serikali za mitaa, watoa huduma za afya ya mifugo na sekretarieti za mikoa wazingatie maelekezo yaliyopo kwenye mwongozo wa utoaji wa chanjo dhidi ya magonjwa ya mifugo nchini na kutoa maoni au kuuliza maswali sehemu ambazo zitakuwa na utata ili kuhakikisha mwongozo huo unatekelezwa kama ambavyo umezingatiwa kwa ajili ya kudhibiti magonjwa ya mifugo nchini.

Ameitaka pia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kutoa nakala za kutosha za mwongozo huo kwa wadau wa sekta ya mifugo kote nchini na pia kuwataka wadau kupata nakala laini kupitia tovuti ya wizara hiyo, www.mifugouvuvi.go.tz.

Awali akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge, Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe. Mwanahamisi Mukunda amesema kuwa mkoa huo utahakikisha yale yote ambayo Wizara ya Mifugo na Uvuvi inatamani yatokee katika Sekta ya Mifugo mkoa upo tayari kuyasimamia ili yalete tija kwa taifa na wafugaji.

“Ili pia mwongozo huu uweze kufanya vizuri kama ya wataalamu wa mifugo bado haitoshi hivyo ni vyema wataalamu waliopo katika ngazi za juu waweze kuwafikia pia wafugaji wa chini na tunataka kuufanya Mkoa wa Dodoma kuwa kitovu cha kuzalisha nyama na maziwa kwa wingi.” Amesema Mhe.Mukunda

Mhe.Mukunda amesema kuwa Sekta ya Mifugo kwa sasa imekuwa ikirasimishwa rasmi na kuifanya iheshimishe watu wanaofanya shughuli za mifugo kwa kuwa imekuwa na tija kubwa kwa taifa na mtu mmoja mmoja.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Pauline Gekul amesema kuwa serikali bado inahakikisha inafanya jitihada mbalimbali za kupata masoko zaidi ya mazao ya mifugo yenye ubora ambayo yanachochewa na uwepo wa chanjo bora na mifugo.

“Wenzangu niwaombe mpokee huu waraka ulipo ukatusaidie ili malalamiko ya mnada umeharibika au wilaya nzima kutokuwa na josho, hayo malalamiko yafike mwisho kupitia mapato mbalimbali ambayo halmashauri wamekuwa wakipata yakiwemo ya minada iliyopo kwenye wilaya hizo, wanapaswa kutenga fedha kwa ajili ya kuyakarabati.” Amefafanua Mhe. Gekul

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji nchini Bw. Jeremiah Wambura amesema kuwa tasnia ya maziwa nchini ikisimamiwa vyema inaweza kuongeza kwa kiasi kikubwa pato la taifa na kuhamasisha uwepo wa viwanda vingi vya kuchakata maziwa nchini.

Hivyo ameiomba Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuangalia vyema namna ya kuisimamia tasnia ya maziwa ili iwe na tija zaidi kwa taifa pamoja na kuongeza wingi wa maziwa ambayo yanaweza kutumika majumbani pamoja na kuchakatwa viwandani.

Mara baada ya uzinduzi wa mwongozo huo Mhe. Ndaki amesema kuwa kuanzia sasa mwongozo huo unaweza kutumika na huduma ya chanjo kuendelea kutolewa na sekta binafsi kwa kushirikiana na serikali.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post